COPA DEL REY:-Picha Namna Neymar alivyoifunga Atletico Mbili na Barcelona Kufuzu Nusu Fainali Jana Januari 28,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, January 29, 2015

COPA DEL REY:-Picha Namna Neymar alivyoifunga Atletico Mbili na Barcelona Kufuzu Nusu Fainali Jana Januari 28,2015.

FC Barcelona imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Mfalme nchini Hipsania ikijulikana kama Copa del Rey  baada ya kuilaza mabao 3-2 Mabingwa wa Hispania Atletico Madrid katika mchezo wa Jana Januari 28,2015, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa bao 4-2.


Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Nou Camp Wiki iliyopita, FC Barcelona waliibuka washindi kwa Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 85 la Staa wao Lionel Messi ambalo alilifunga baada ya Penati yake kuokolewa na Kipa na Mpira kumrudia tena na kuukwamisha wavuni na hivyo Barcelona kusonga Nusu Fainali na watakutana na Mshindi kati ya Getafe na Villareal ambao katika Mechi yao ya kwanza, Villareal alishinda Bao 1-0.

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Fernando Torres aliifungia Atletico dakika ya kwanza ya mchezo , kabla ya Barcelona kusawazisha dakika ya tisa.

Kisha Penati ya Raul Garcia ikawapa Atletico Bao la Pili lakini Beki wao Miranda akajifunga mwenyewe na Neymar akaipa Barca Bao la 3 na la ushindi.

Balaa kwa Atletico lilikuja pale Gabi alipopewa Kadi Nyekundu wakati wa Haftaimu Wachezaji wakielekea Vyumba vya Kubadili Jezi na Mario Suarez kufuatia mwishoni.

Neymar akishangilia Uwanja wa Vicente Calderon baada ya kuiungia mabao maili katika ushindi wa 3- na Atletico Madrid.
 
Alhamisi Januari 29,2015.

2200 Getafe v Villareal [0-1]

0001 Sevilla v Espanyol [1-3]

0001 Atletic Bilbao v Malaga [0-0]

NUSU FAINALI

Februari 11 & Machi 4,2015.

Malaga/Athletic Bilbao v Espanyol/Sevilla

Villareal/Getafe v Barcelona

FAINALI

Mei 30,2015.


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad