CAPITAL ONE CUP:- Fainali Wembley March 01,2015 Chelsea V/s Tottenham. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, January 29, 2015

CAPITAL ONE CUP:- Fainali Wembley March 01,2015 Chelsea V/s Tottenham.

Tottenham jana Januari 28,2015 usiku wametoka na ushindi wa  Sare 2-2 na Sheffield United kwenye Marudiano ya Nusu Fainali ya Capital One Cup na kutinga Fainali  watakayocheza Wembley na Chelsea.

 Tottenham wamesonga kwa Jumla ya Mabao 3-2 baada ya ushindi katika Mechi yao ya kwanza iliyochezwa pia Wiki iliyopita huko White Hart Lane, walipoifunga Sheffield United Bao 1-0 kwa Bao la Penati iliyotolewa Dakika ya 75 baada ya Jay McEveley kuushika Mpira na Andros Townsend kupiga Penati hiyo na kufunga.



Hapo Januari 27,2015, Chelsea walitinga Fainali baada ya kuifunga Liverpool 1-0 na kutinga Fainali kwa Jumla ya Mabao 2-1.

Hapo Jana, Sheffield United walifunga Bao zao zote 2 kupitia Che Adams na Tottenham kufunga zao kupitia Christian Eriksen.

CAPITAL ONE CUP RATIBA

FAINALI

Jumapili 1 Machi 2015

Chelsea v Tottenham

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad