AFCON 2015:- Picha 5 jinsi Ivory Coast ilivyofuzu Jana Pamoja na Ratiba ya Mechi za robo fainali Jumamosi Januari 31,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, January 29, 2015

AFCON 2015:- Picha 5 jinsi Ivory Coast ilivyofuzu Jana Pamoja na Ratiba ya Mechi za robo fainali Jumamosi Januari 31,2015.

KUNDI D la Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, limemaliza Mechi zao za mwisho jana Januari 28,2015 na Ivory Coast kutinga Robo Fainali baada ya kuifunga Cameroun lakini Mali na Guinea zinangoja kurushwa Shilingi kuamua nani ataungana nao baada ya Timu hizo kutoka Sare kwenye Mechi yao ya mwisho na kufungana kwa kila kitu.


Kwenye mchezo huo huko Nuevo Estadio de Malabo, Mjini Malabo Ivory Coast wametinga Robo Fainali baada ya mapumziko kuongoza wakiwa Bao 1-0 mbele kwa Bao la Dakika ya 36 la Max-Alain Gradel kwa Shuti la Mita 30.


Kwenye mchezo wa GUINEA V/s MALI huko Estadio de Mongomo, Mjini Mongomo,Guinea walitangulia kupata Bao lao kwa Penati iliyotolewa Dakika ya 13 kufuatia Wague kuunawa Mpira na Kevin Constant kufunga Penati hiyo.

Mali walishindwa kusawazisha Dakika chache baadae baada ya wao pia kupewa Penati kufuatia Issiaga Sylla kuunawa lakini Seydou Keita alipiga Penati dhaifu iliyookolewa na Kipa Naby Yattara.

Kipindi cha Pili Modibo Maiga, Mchezaji wa West Ham anacheza kwa Mkopo Metz ya France, aliawazisha kwa Mali kwa Kichwa baada ya Krosi ya Abdoulay Diaby.

AFCON 2015 RATIBA.

**Saa za Bongo

ROBO FAINALI

Jumamosi Januari 31,2015

1900 Congo v Congo DR Kundi B [Estadio de Bata]=RF1  
   
2200 Tunisia v Equatorial Guinea [Estadio de Bata]=RF2

Jumapili Februari 1,2015

1900 Ghana v Guinea au Mali [Estadio de Mongomo]=RF3 
  
2200 Ivory Coast v Algeria [Nuevo Estadio de Malabo]=RF4  
  
NUSU FAINALI

Jumatano Februari 4,2015

2200 RF 1 v RF4 [Estadio de Bata]=NF1

Alhamisi Februari 5,2015

2200 RF2 v RF3 [Nuevo Estadio de Malabo]=NF2 
     
MSHINDI WA 3

Jumamosi Februari 7,2015

2100 Aliefungwa NF1 v Aliefungwa NF2 [Nuevo Estadio de Malabo]

FAINALI

Jumapili Februari 8,2015

2200 Mshindi NF1 v Mshindi NF2 [Estadio de Bata]    

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad