AFCON 2015:- Januari 20- Ivory Coast 1-1 Guinea baada ya Gervinho kulimwa kadi Nyekundu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 20, 2015

AFCON 2015:- Januari 20- Ivory Coast 1-1 Guinea baada ya Gervinho kulimwa kadi Nyekundu.

Ivory Coast imepata sare ya goli 1-1  dhidi ya Guinea katika kombe la mataifa ya Afrika 2015 baada ya Guinea kuwa wa kwanza kupata bao licha ya mshambuliaji  Gervinho kupewa kadi nyekundu katika mchezo huo wa leo Januari 20,2015.

Mchezo huo wa kundi D la AFCON 2015,Guinea ilichukua uongozi kunako dakika ya 36 baada ya Mohammed Yattara kucheka na wavu.

Aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal, Gervinho ambaye mkwaju wake ulipiga mwamba wa goli la Guinea katika kipindi cha kwanza alipewa kadi nyekundu na hivyo  kutoka nje katika dakika ya 58 kwa kosa la utovu wa nidhamu la kumpiga mchezaji mwenzake.

Mcheza Traore wa Guinea karibia apate bao la pili wakati kombora lake lilipogonga mwamba wa goli, lakini IvorY Coast ilijiokoa baada ya Seydou Doumbia Kufunga katika eneo la hatari.

Usiku huu wa saa NNE ipo  mechi kati ya Mali na Cameroon.

2200 Mali v Cameroon [Nuevo Estadio de Malabo] 
    
Jumatano Januari 21,2015.

KUNDI A

1900 Equatorial Guinea v Burkina Faso [Estadio de Bata]
                
2200 Gabon v Congo [Estadio de Bata]   
        
Alhamisi Januari 22,2015.

KUNDI B

1900 Zambia v Tunisia [Nuevo Estadio de Ebebiyín]   

2200 Cape Verde Islands v Congo DR [Nuevo Estadio de Ebebiyín]           

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad