 |
|
DR Congo
ilitoka nyuma na kuishinda Congo kwa mabao 4-2 huko Estadio de Bata Mjini Bata
Nchini Equatorial Guinea na kutinga Nusu Fainali ya AFCON 2015.
Robo Fainali
za AFCON 2015, Kombe la Mataifa ya Afrika,iliwashuhudia Congo DR iliyotoka
nyuma 2-0 na kuishinda Congo katika mechi iliokuwa na kasi na mchezo mzuri
kutoka pande zote mbili.
Ferebory
Dore alifunga krosi safi huku Thievy Bifouma akifunga pia na kuwa mabao 2-0.
Katika
dakika ya 16 Diermerci Mbokani alifunga bao la kwanza ,kabla ya Bolika kufunga
bao la pili naye Joel Kimuaki akafunga bao la tatu.
|
 |
|
Wachezaji wa
Congo wakisherehekea ushindi.
|
 |
|
Mbokani
aliwazunguka tena mabeki wa Congo na kufunga bao la nne na la ushindi katika
shambulizi la ghafla.
Baadae Usiku
huu ipo Mechi nyingine ya Robo Fainali kati ya Wenyeji Equatorial Guinea na
Tunisia.
Hapo Kesho Februari
01,2015,Robo Fainali itakamilika kwa Ghana na Guinea kucheza huko Estadio de
Mongomo Mjini Mongomo na kufuatiwa na Ivory Coast na Algeria huko Nuevo Estadio
de Malabo Mjini Malabo.
Washindi wa
Mechi hizo 4 watatinga Nusu Fainali.
|
Jumapili
Februari 1,2015.
1900 Ghana v
Guinea [Estadio de Mongomo]
2200 Ivory
Coast v Algeria [Nuevo Estadio de Malabo]
NUSU
FAINALI
Jumatano
Februari 4,2015.
2200 Congo
DR v Ivory Coast/Algeria [Estadio de
Bata]=NF1
Alhamisi
Februari 5,2015.
2200
Tunisia/Equatorial Guinea v Ghana/Guinea [Nuevo Estadio de Malabo]=NF2
MSHINDI
WA 3
Jumamosi
Februari 7,2015.
2100
Aliefungwa NF1 v Aliefungwa NF2 [Nuevo Estadio de Malabo]
FAINALI
Jumapili
Februari 8,2015.
2200 Mshindi
NF1 v Mshindi NF2 [Estadio de Bata]
No comments:
Post a Comment