SOMA HAPA:-Mkusanyiko wa zile Stori muhimu zilizopewa nafasi kwenye Magazeti ya leo December 15, 2014 - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, December 15, 2014

SOMA HAPA:-Mkusanyiko wa zile Stori muhimu zilizopewa nafasi kwenye Magazeti ya leo December 15, 2014

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Kigagila, jijini Dar es Salaam, wakizozana na mmoja wa maafisa wa uchaguzi kata ya Kiwalani, kufuatia tangazo la kuahirishwa kwa uchaguzi kutokana na dosari zilizoibuka wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa katika eneo hilo jana Desemba 14,2014. Picha na Oma Fungo

MWANANCHI

Mgombea Uenyekiti kupitia Chama cha CCM Mtaa wa Swea kata ya Mkolani Mwanza Pius Mihayo amefariki dunia gafla akiwa mtaani kwake muda mfupi baada ya kupiga kura.

Msimamizi wa uchagyzihuo Halifa Hida alisema mgombea huyo alifariki dunia gafla akiwa kwenye mtaa wake wa Swea na chanzo cha kifo chake hakijajulikana.

“Sasa kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi,tutatangaza matokeo ya wajumbe na nafasi za wagombea wa vitimaalum,nafasi ya uenyekiti haitatangazwa hadi taratibu nyingine za uchaguzi zitakapoandaliwa”alisema Hida.

Mkoani Arushamsongamano wa wapigakura katika kituo chaMbauda kata ya Sombetini unadaiwa kusababisha kifo cha mtu aliyetambulika kwa jina la Suleiman Bakari.

Tukio hilo lilitokea saa 3 asubuhi katika kituo hicho ambacho kilikua kimefurika watu ambapomtu huyo alianguka gafla baadaya kukosa hewa akiwa kwenye mstari wa kupigakura.

NIPASHE

Uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji ulifanyika nchini kote jana huku ukitawaliwa na kasoro na vurugu kubwya  zilizosababishapolisi kutumia risasi za moto na baadhi ya wapigakura kuchapana makonde jijini Dar es salaam.

Vurugu hizo zilitokana na uchaguzi huo kugubikwa na kasoro nyingi na hivyo kusababisha baadhi ya vituo kulazimika kuahirisha uchaguzi huo hadi wiki ijayo.

Baadhiya kasoro zilizoibuka zilitokana na baadhi yavituo kuchanganya majina ya wagombea,kuchelewa kuanza kwa uchaguzi,kukosekana kwa vifaa vya kupigia kura pamoja na baadhi ya wagombea kuwahujumu wengine.

Uchaguzi huo ulipangwa kuanza saa2 asubuhi lakini maeneo mengi ulichelewa kuanza kutokana na vifaa kuchelewa kufika vituoni.

Katika kituo cha Kimara bucha kulitokea vurugu kubwa baada ya mawakala kugombea kuwasaidia wapigakura kuweka alama ya vyema kwa wagombea na baadhi ya watu kutakakurudia kup[iga kura hali iliyosababisha msimamizi wa kituo hicho kupigwa na wapigakura kutokanana na kukerwa na kitendo cha baadhi yawatu kurudia kupiga kura.

NIPASHE

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga mjini amevamiwa na kundi la vibaka wakati akienda Zahanati kupatiwa matibabu na kisha kuporwa vitu mbalimbali mjini Shinyanga.

Masele alisema tukio hilo lilitokea juzi saa4 usiku wakati akienda kupatiwa matibabu ya matatizo ya koo katika Zahanati ya Bakwata  na gafla alivamiwa na kundi la watu wapatao 30 na kumpora mali zake.

Alisema akiwa na Naibu Katibu mkuu CCM Zanzibar,Vuai Aly wakipata chakula cha usiku hotelini gafla alijisikia vibaya na kuamua kwenda kwenye Zahanati hiyo kupatiwa matibabu na ndipo alipata mkasa huo wakati akiwa njiani.

Masele alikanusha tuhuma alizozushiwa na wananchi kuwa kuporwa huko kunatokana na yeye kugawa rushwa kwa wananchi wakati wa kampeni Serikali za mitaa ili wananchi wawachague wagombea wa CCM.

MTANZANIA

Katibu wa CCM kata ya Narungombe Lindi Mohamed Pilipili amevamiwa na kupigwa hadi kuzimia na mabaunsa kwa madai ya kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba usiku.

Tukio hilo lilitokea juzi usiku katika kitongoji cha Chikwale baada ya kundi la mabaunsa kumvamia na kumpiga Katibu huyo pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo Seleman Lukuche.

Akizungumzia tukio hilo Lukeche alisema ilikua saa 3 usiku wakitoka Ruangwa kupeleka taarifa za mwenendo wa uchaguzi pamoja na majina ya mawakala wa CCM ndipo walipovamiwa na kundi hilo la mabaunsa10waliodai wao wanadhibiti .vitendo vya ryushwa ambao walianza kuwapiga bila kutaka maelezo.

Katika tukio jingine mgombea wa nafasi ya uenyekiti kata ya Mkwajuni amepigwa na watu wanaodaiwa wafuasi wa CUF kwa madai kuwa alikwenda kwenye eneo la Mjimwema kupanga mikakati ya kuiba kura.

UHURU

Muda wowote kuanzia sasa Rais Jakaya Kikwete atatoa na kutangaza uamuzi wake kuhusiana na baadhi ya watendaji wakiwemo Mawaziri kuhusishwa katika kashfa ya wizi wa fedha za Tegeta Escrow.

Wiki iliyopita Rais alipokea na kupiia ripoti iliyowasilishwa kwake,nyaraka na ushauri uliotolewa katika maazimio ya Bunge kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow.

Kikwete ambaye alianza kazi Desemba 8 mwaka huu baada ya mapumziko kutokana na kufanyiwa upasuaji alisema atatoa uamuzi wake ndani ya wiki hii.

Alisema atatolea maamuzi mambo ambayo yanamuhusu yeye moja kwa moja na yale yanayohusu Serikali atatolea uamuzi na maelekezo ya namna ya kuyashughulikia.

Bunge lilitoa maazimio mbalimbali kwa Serikali ikiwemo kuitaka mamlaka ya uteuzi  kuwawajibisha ikiwani pamoja na kuwavua nyadhifa zao Waziri wa Nishatina Madini,Mwanasheria mkuu,Waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi,Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na madini na wengineo.

HABARILEO

Kundi la watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wamevamia na kupora fedha na vitu mbalimbali ndani ya kanisa Katoliki la Kilema jimbo la Moshi vijijini Mkoani Kilimanjaro.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuakia jana ambapo watu hao wakiwa na vifaa maalum  vya kuvunja milango,walivunja langokuu la kanisa hilo na kuvunja sanduku la sadaka na kupora vifaa vya kufanyia ibada.

Padri wa Parokia ya Kilema DamianTemere alisema vitu vilivyoibwa ni pamoja na vifaa vitakatifu vinavyotumika katika sikukuu ya Ekaristi na majambazi hayo yalivunja kasha la kuhifadhia sadaka na kupora fedha zilizokuwemo ambazo hazikujulikana thamani yake.

Alisema pia waliiba vifaa vya kunywea divai na kumunio ambavyo nivya dhahabu vyenye thamani ya mamilioni ya fedha huku wakiacha vile vya shaba.

Alisema baadhi ya vifaa hivyo vilinunuliwa na wamisionari wa kwanza na vilikua na thamani kubwa kwa kanisa hilo kwa kuwa niliwakilisha imani katika parokia hiyo na kanda nzima ya Kaskazini.

MWANANCHI

Shirika la usafiri wa anga la China Avic International liko kwenye mazungumzo na Shirika la ndege la hapa nchini ATCL ili kuliwezesha Shirika hilo la Tanzania kufanya kazi kwa ufanisi.

Avic inayomilikiwa na Serikali ya China imesema mkakati wake wa kwanza ni kutoa ndege kwa ATCL ili kuboresha huduma zake,kufanya kazi na kujiendesha kama ilivyo kwa mashirikayandege ulimwenguni.

Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya UchukuziMonica Mwamunyange alisema kituo hicho kimeanzishwa baada ya makubaliano ya nchi mbili yaliyofanyika China mwezi Oktoba mwaka huu wakati Kikwete alipotembelea nchi hiyo.

“Tuliangalia suala la kuunganisha nguvu kati ya ATCL na Avic International na tayari wenzetu wa China wameamua kuanzisha kituo hiki”alisema Mwamunyange.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad