Vanessa Mdee akiwa na tuzo yake ya Best Female
Artist in East Africa 2014.
Mwanamuziki wa Tanzania Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa kuamkia
leo Desemba 28,2014, ametwaa tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kiume Afrika Mashariki
(Best Male Artist in East Africa) kutoka Tuzo za 2014 AFRIMA zilizofanyika huko
jijini Lagos nchini Nigeria.
Mwanadada
Vanessa Mdee yeye ameshinda tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika Mashariki
(Best Female Artist in East Africa).
Tuzo ya
Diamond imepokelewa na mwanamuziki Peter Msechu aliyekuwepo katika zoezi hilo
la utoaji tuzo maana na yeye alikuwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo
hizo.
|
so beautyful, thanks for sharing
ReplyDelete