Wakati Taifa likikabiliwa na changamoto kubwa
ya uhaba wa dawa hospitalini, aina mpya na hatari zaidi ya ugonjwa wa kifua
kikuu sugu imegundulika na kuathiri mtu mmoja nchini.
Mgonjwa huyo alibainika kuwa na kifua kikuu
sugu kisicho na tiba, aina ya ‘Xtreme Drug Resistant’ au XDR-TB ambayo hapo
awali haikuwa ikiwaathiri Watanzania.
Huyu ni mgonjwa wa pili kubainika kuwa na
aina hii hatari ya TB baada ya kesi ya kwanza kuripotiwa mwaka 2011.
Shirika la Afya Duniani (WHO) linaeleza kuwa
XDR-TB ni nadra sana ambapo ni nchi 77 tu duniani ikiwamo Tanzania zimeripoti
tatizo moja moja, mwishoni mwa mwaka 2011.
Taarifa zilizokusanywa na WHO kutoka katika
mataifa mbalimbali duniani zinahakiki kuwa kuna asilimia tisa tu ya kesi za
XDR-TB.
MDR-TB ni kifua kikuu sugu ambacho
kimeshindikana kutibika kwa dawa za mstari wa pili.
Mratibu wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu Mkoa wa
Kinondoni, Dk Hassan Lupinda alithibitisha kupokewa kwa mgonjwa huyo na kusema
kuwa alipokelewa katika Hospitali ya Mwananyamala na vipimo pamoja na historia
yake ilibainisha kuwa ana TB aina ya XDR.
“Ni kweli tumempokea mgonjwa huyo ambaye ni
Mtanzania aliyekuwa akitokea Afrika Kusini, na sasa tayari tumempeleka
Kibong’oto wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kwa matibabu,” alisema.
Wakati huohuo, takwimu za Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii Nchini zinaonyesha kuwa kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wa
kifua kikuu ambapo idadi ya watu waliopimwa mwaka 2013 imeongezeka kutoka 11,
640 mwaka 2009 hadi 20,469,241 mwaka 2013.
|
thanks for sharing
ReplyDelete