![]() |
Ujenzi wa
Maabara wa Vyumba vitatu umekamilika kwa kiasi kikubwa katika shule ya Sekondari Nyabisindu
iliyopo kata ya Kabanga (Pichani) wilayani Ngara mkoani Kagera hali itakayosaidia wanafunzi wa shule hiyo
kusoma kwa nadharia na vitendo hasa masomo ya Sayansi kwa rahaa tupu.
Diwani wa
Kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera,Bw. Soud
Saidr amewapongeza Wananchi wa kata
hiyo kwa Ushirikiano wao katika Ujenzi huo wa Maabara kwani katika Kata hiyo
tayari ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 100 kwa Shule ya Sekondari Kabanga
na sasa Nyabisindu.
|
![]() |
Picha hii
ilipigwa Desemba 05,2014 wakati uezekaji wa bati ulipokamilika sambamba na upigaji ripu katika Shule ya
Sekondari Nyabisindu , Kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera.
|
![]() |
UNGANANASI
KATIKA FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment