LA LIGA 2014/2015:-Taswira ya FC Barcelona wakicheza Nou Camp na kutandika 5 – 0 timu toka mkiani Cordoba. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 21, 2014

LA LIGA 2014/2015:-Taswira ya FC Barcelona wakicheza Nou Camp na kutandika 5 – 0 timu toka mkiani Cordoba.

FC Barcelona, Jana Desemba 20,2014, wakicheza kwao Nou Camp, wameibamiza Timu ya Pili toka mkiani Cordoba Bao 5-0.

 Matokeo haya yameifanya Barcelona kuwakaribia Vinara wa La Liga Real Madrid wakiwa Pointi 1 nyuma yao ingawa wao Barcelona wamecheza Mechi 1 zaidi.

Real Madri hivi sasa wako Nchini Morocco na wamecheza Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu dhidi ya San Lorenzo ya Argentina na kushinda taji hilo kwa ushindi wa bao 2-0.



Hapo Jana Desemba 20,2014, Bao za Barcelona zilipachikwa na Pedro, Dakika ya Pili, Luis Suarez, 53, Gerard Pique 80 na Bao 2 za Lionel Messi, Dakika za 82 na 90.

Hii ndio Mechi yao ya mwisho ya La Liga kwa Mwaka huu kwa Barcelona kwani Ligi hiyo inaenda mapumziko ya Krismasi na itarejea kilingeni hapo Januari 3,2015.

Ijumaa Desemba 19,2014.

Celta de Vigo 0 – 1 UD Almeria 

Jumamosi Desemba 20,2014.

Barcelona 5 – 0  Cordoba 

Levante 1 - 1 Real Sociedad

Eibar 0 - 1 Valencia

Rayo Vallecano 1 - 3 Espanyol

Jumapili Desemba 21,2014.

1400 Villarreal v Deportivo La Coruna

1900 Granada v Getafe

2100 Elche v Malaga

2300 Athletic Bilbao v Atletico Madrid


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad