PICHA YETU YA LEO DESEMBA 21,2014:-Ni kuhusu Harakati ya Kisiasa wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 21, 2014

PICHA YETU YA LEO DESEMBA 21,2014:-Ni kuhusu Harakati ya Kisiasa wilayani Ngara mkoani Kagera.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwigulu Nchemba akiwasili mjini Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera Desemba 13,2014 kwa ziara ya Kichama ya siku moja.



Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwigulu Nchemba akiwasili mjini Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera Desemba 13,2014 ambapo alipokelewa na Kostantine Kanyasu (Mkuu wa wilaya ya Ngara) wanaekumbatiana  wakati wa ziara yake ya siku moja ya kichama wilayani Ngara mkoani Kagera kuhamasisha uhai wa chama na kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa za chama hicho.Picha na Shabani Ndyamukama.








Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwigulu Nchemba akiwahutubia wakazi wa Mji wa Rulenge ,wilayani Ngara mkoani Kagera Desemba 13,2014 .Pamoja na mambo mengine aliwataka wananchi kuendelea kuiamini serikali ya CCM hasa wakati huu taifa likiwa kwenye sakata la Escrow na kuahidi wale wote wanaofuja mali za umma watashughulikiwe kwa mujibu wa sheria na taratibu za Nchi.




Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwigulu Nchemba alipowasili mjini  Ngara,alifanya pia mkutano wa Haradha katika viwanja vya posta ya zamani   wakati wa ziara yake ya siku moja ya kichama wilayani Ngara mkoani Kagera Desemba 13,2014 kuhamasisha uhai wa chama na kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa za chama hicho.


Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu na Mbunge wa Jimbo la Ngara mkoani Kagera ,Deogratius Ntukamazina wakiwa jukwaani wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwigulu Nchemba wilayani Ngara mkoani Kagera Desemba 13,2014.


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad