KLABU BINGWA DUNIANI 2014:-Ni Real Madrid ya Hispania……Tazama Picha 9 walivyolibeba Kombe ! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 21, 2014

KLABU BINGWA DUNIANI 2014:-Ni Real Madrid ya Hispania……Tazama Picha 9 walivyolibeba Kombe !


Unaweza kusema kweli huu ni mwaka wa Real Madrid, kwani wamefanikiwa kuitwanga San Lorenzo kwa mabao 2-0 na kubeba Ubingwa wa Dunia kwa msimu huu wa 2014/2015.

Real Madrid wametupia mabao hayo mawili hapo jana Desemba 20,2014, kupitia kwa Sergio Ramos na Gareth Bale na kubeba Kombe hilo katika ardhi ya bara la Afrika.

Mechi hiyo ya fainali ya Kombe la Dunia kwa klabu, imepigwa mjini Marakech, Nchini Morocco.

Hivi sasa Real Madrid wapo kwenye wimbi la ushindi wa Mechi 22 mfululizo na wanaikimbiza Rekodi ya Dunia ya kushinda Mechi 24 mfululizo inayoshikiliwa na Klabu ya Brazil, Curitiba, waliyoiweka Mwaka 2011.



Cristiano Ronaldo hakuweza kufunga katika mechi hiyo ambayo Madrid imeshinda mara 22 mfululizo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Real kutwaa Kombe hili ambalo ni Mashindano ya FIFA ingawa wameshawahi kutwaa Intercontinental Cup mara 3 ambalo lilikuwa likifanana na hili ingawa hilo lilishindaniwa na Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Mabingwa wa Marekani ya Kusini tu.



Real Madrid  pia wamekamataTaji lao la 4 kwa Mwaka 2014 kitu ambacho walikuwa hawajahi kukifanya baada ya kuwahi kutwaa Mataji Matatu tu ndani ya Mwaka mmoja lakini Mwaka huu 2014 wamefanikiwa kubeba UEFA CHAMPIONZ LIGI, Copa del Rey, UEFA SUPER CUP pamoja na Kombe la FIFA la Klabu Bingwa Duniani.

Vile vile wamemaliza Mwaka 2014 kwa kuwa Vinara wa Ligi ya kwao Spain La Liga wakiwa Pointi 1 mbele ya Mahasimu wao FC Barcelona ambao wamecheza Mechi moja zaidi.

Mapema hiyo Jana Desemba 20,2014, kwenye Mechi ya kusaka Mshindi wa 3, Auckland City ya New Zealand iliishinda Cruz Azul kwa Mikwaju ya Penati 4-2 baada ya Sare ya Bao 1-1.



UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad