EPL 2014/2015:- Matokeo ya mechi za Leo Desemba 20, Man United na Man City haya hapa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 20, 2014

EPL 2014/2015:- Matokeo ya mechi za Leo Desemba 20, Man United na Man City haya hapa.

Bao 3 za Kipindi cha Pili zimewapa ushindi wa 3-0 Mabingwa Manchester City walipocheza na Crystal Palace leo Desemba 20,2014 ,wakiwa kwao Etihad na kuikamata Chelsea kwa Pointi kileleni mwa Ligi Kuu Uingereza msimu huu wa 2014/2015.

Sasa Chelsea na Man City zote zina Pointi 39 lakini Chelsea wanabaki Nambari Wani wakiwa na ubora wa tofauti ya Magoli na pia wana Mechi moja mkononi ambayo watacheza Jumatatu Usiku Ugenini na Stoke City.


Kwenye Mechi ya Leo Desemba 20,2014, Man City, wakicheza bila ya Sentafowadi anaetambulika kutokana na kuumia kwa Masentafowadi wao Sergio Aguero na Edin Dzeko, walitoka 0-0 hadi Mapumziko.

Lakini Kipindi cha Pili, Bao 2 za David Silva na Yaya Toure ziliwapa ushindi waba Bao 3-0 dhidi ya Palace.


Manchester United wameendelea kukamata Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 7 nyuma ya Vinara Chelsea na Man City baada ya Leo Desemba 20,2014 kupata Sare ya 1-1 Ugenini huko Villa Park walipocheza na Aston Villa.

Villa walitangulia kufunga katika Dakika ya 18 kwa Bao la Christian Benteke lakini Radamel Falcao aliisawazishia Man United katika Dakika ya 53.

Villa walibaki Mtu 10 baada ya Agbonlahor kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 65 kwa kumchezea Rafu mbaya Ashley Young.

Ligi Kuu Uingereza  itaendelea Jumapili Desemba 21,2014 kwa Mechi mbili na Jumatatu Mechi moja.

Jumapili Desemba 21,2014.

1630 Newcastle v Sunderland    
           
1900 Liverpool v Arsenal    
        
Jumatatu Desemba 22,2014.

2300 Stoke v Chelsea
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad