Barua ya shukrani kwa Kampuni ya Tanzania
Environment & Conservation (TECO) inayomilikiwa na Masweta.
Na
Johnson James, Mwanza.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Bw.Halifa Hassan Hida ameingia katika kashfa nzito
baada ya mwanaharakati aliyefahamika kwa jina la John Masweta kutinga kwenye
geti kuu la Makao Makuu ya Jiji la Mwanza jana Desemba 22,2014 huku akiwa amevaa gunia
kumshinikiza mkurugenzi huyo amlipe shilingi 1,600,000 aliyopewa kama zawadi na
uongozi wa mkoa na mkurugenzi huyo kushindwa kuilipa fedha hiyo kwa wakati.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Mwanza kwenye lango kuu la kuingia ofisi za jiji
hilo, Masweta alisema kuwa yeye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kampuni
ya Tanzania Environment & Conservation (TECO) aliyejitolea kwa zaidi
ya miaka 20 kupanda miti na amekuwa akipewa tuzo mbalimbali kutokana na kazi
hiyo na kuweza kuliokoa taifa katika majanga ya jangwa.
Masweta
ameendelea kufafanua kuwa katika kuhakikisha analisaidia taifa, amepanda miti
katika maeneo mbalimbali jijini Mwanza na wakati akiendelea kupanda miti hiyo
akawa amepatiwa tuzo ya mwanaharakati bora kwa kutunza mazingira iliyoambatana
na fedha taslimu shilingi milioni moja na laki sita lakini cha kushangaza
mkurugenzi amekataa kutoa fedha hiyo na badala yake amempatia cheti tu bila kumpatia
na fedha.
Katika hatua
nyingine, Masweta ameendelea kusema kuwa yeye hakupanda miti kwa lengo la
kulipwa na taifa bali alipanda miti ili kuliondoa taifa katika janga la
kukumbwa na jangwa lakini cha kushangaza kila anapotiwa moyo kwa kupatiwa
fedha kidogo, fedha hiyo huishia mikononi mwa watu wengine ambao hawana huruma
na maisha yake.
Hata hivyo,
Masweta alikuwa na mabango yaliyoandikwa ujumbe mbalimbali kama Toa nguvu
zako kwa kulitumikia taifa, uwe faida kwa jamii na taifa, onea huruma
tumbo lako kula mpaka sisimizi, Udhalimu wa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
haukubaliki.
Masweta
amesema kuwa hatoki kwenye lango hilo hadi pale mkurugenzi huyo atakapompatia
kiasi hicho cha fedha anazodai.
Aidha
Masweta ametoa rai kwa raia kwa kusema kuwa yeye ni mgonjwa wa kisukari na
hajanywa maji yoyote tokea asubuhi endapo akifariki basi wafahamu kwamba
aliyesababisha kifo chake ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kutokana na kuwa na
nia ya kudhulumu haki za wenzake.
|
No comments:
Post a Comment