AJALI:-Watu wanne wamefariki na wengine watano wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Uchira. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, December 31, 2014

AJALI:-Watu wanne wamefariki na wengine watano wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Uchira.

Watu wanne wamefariki papo hapo na wengine watano wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea leo mchana eneo la Uchira katika barabara kuu ya Moshi/Dar baada ya bus la kampuni ya kilenga kupasuka tairi na kuyumba barabarani na kugongana na bus dogo aina ya toyota hiace. 

Walioshuhudia ajali hiyo wamesema imetokea saa saba mchana wakati basi hilo aina ya Costa lililokuwa likitoka Moshi kwenda Same kugongana na basi dodo aina ya Toyota Hiace ambalo lilikuwa linatoka Moshi kwenda Mwanga.


Wamesema, dreva wa bus dogo alishindwa kulikwepa bus la kilenga na kwenda kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu hao waliokuwa ndani ya Toyota hiace. 

Muuguzi wa zamu wa hospitali ya rufaa ya KCMC Bi Justine Haule amethibitisha kupokea miili ya marehemu wanne akiwemo mwanamke mmoja na wanaume watatu na majeruhi wanawake wanne na mwanamme mmoja.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Bw Godfrey Kamwela amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na jeshi la polisi linaendelea kukusanya taarifa na kufanya uchunguzi zaidi na kutoa taarifa kwa umma.

Picha/Habari :-ITV.
 
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad