KIFO CHA SENZO MEYIWA:-Maelfu wamzika leo November 1, 2014,Africa Kusini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, November 01, 2014

KIFO CHA SENZO MEYIWA:-Maelfu wamzika leo November 1, 2014,Africa Kusini.


Jeneza la Senzo Meyiwa.

Maelfu ya watu wamehudhuria mazishi ya aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya Afrika Kusini Senzo Meyiwa yaliyofanyika jijini Durban Jumamosi hii November 01,2014.


Meyiwa, mwenye umri wa miaka 27, alipigwa risasi Jumapili iliyopita,October 26,2014 baada ya majambazi kuingia nyumbani mwa mpenzi wake karibu na Johannesburg.


Senzo Meyiwa akiokoa mchomo katika moja ya mechi alizocheza wakati wa uhai wake.

Mtuhumiwa wa mauaji ya Meyiwa alifikishwa mahakamani Ijumaa October 31,2014 na alishitakiwa kwa mauaji dhidi ya mlinda mlango huyo maarufu nchini Afrika Kusini.

Kifo cha Meyiwa kilisababisha mshituko mkubwa nchini Afrika Kusini na yameonyesha kiwango cha juu cha uahlifu wa kutumia nguvu nchini humo.

Mazishi yanafanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Moses Mabhida Stadium katika mji wa Durban nyumbani kwa Meyiwa.

Wengi wa waombolezaji wamevaa fulana zenye picha ya Meyiwa, mtu ambaye alikuwa kivutio kikubwa kimichezo.

Bendera nusu mlingoti.

Rais Zuma ameamuru bendera ya taifa ipepee nusu mlingoti siku hii ya Jumamosi ili kumuenzi mlinda mlango huyo wa timu ya taifa.

Polisi wamesema Ijumaa October 31,2014,kuwa mtuhumiwa wa mauaji ya Meyiwa alitambuliwa katika gwaride la utambuzi.

Mtuhumiwa huyo, Zanokuhle Mbatha, mwenye umri wa miaka 25, anakabiliwa na mashitaka ya mauaji na ujambazi wa kutumia silaha na anatarajiwa kufikishwa tena mbele ya mahakama Novemba 11,2014.

Polisi wametangaza zawadi kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa zaidi kuhusu shambulio hilo ili kuwanasa watuhumiwa wengine.

Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad