AJALI NYINGINE:-Ni Lori na Basi la abiria kugongana uso kwa uso wilayani Kahama,mkoani Shinyang’a. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, November 01, 2014

AJALI NYINGINE:-Ni Lori na Basi la abiria kugongana uso kwa uso wilayani Kahama,mkoani Shinyang’a.

Mtu mmoja anasemekana kupoteza maisha na mwingine kujeruhiwa baada ya Magari Mawili waliyokuwa wanaendesha kugongana uso kwa uso katika eneo la Trans Oil, kata ya Nyasubi Wilayani Kahama mkoani Shinyanga usiku wa October 31,2014.

 Tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku huu likihusisha gari aina ya Coster mali ya Kampuni ya CK Safari Tours yenye namba T-468-CAL kugongana na Semi Teller aina ya Scania yenye namba T-498-BVH.

Kwa mujibu wa Mashuhuda, gari aina ya Coster ilikuwa ikitokea eneo la kituo cha Mafuta kwenda Phantom, huku Scania hiyo ikitokea jijini Dar-es-salaam kwenda nchi jirani na ndipo zikagongana uso kwa uso. 

Taarifa zinasema Dereva wa Scania hiyo ndiye huenda amefariki dunia huku dereva wa Coster hiyo akisemekana kujeruhiwa na kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu. 

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika, na tayari Jeshi la polisi wilayani Kahama lilimefika katika eneo la tukio na taratibu za kuyatoa magari hayo katikati ya barabara zilifanyika.

Na:- DUNIA KIGANJANI-Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad