LIGI KUU TANZANIA BARA 2014/2015:- Simba sare tena,Yanga SC na Azam FC zapigwa 1-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, November 01, 2014

LIGI KUU TANZANIA BARA 2014/2015:- Simba sare tena,Yanga SC na Azam FC zapigwa 1-0.

Wekundu wa Msimbazi Simba SC imetoa sare ya sita mfululizo tangu kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu wa 2014/2015, baada ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro jioni ya leo November 1, 2014.

Ushindi huo, unawafanya Mtibwa wafikishe pointi 14 kileleni mwa ligi hiyo, wakati Simba SC inaokota pointi ya sita baada ya timu zote kucheza mechi sita. 

Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa tayari inaongoza kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na beki wa kimataifa wa Uganda, Joseph Owino dakika ya 35 kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Emmanuel Okwi.
Kipa Peter Manyika alifanya kazi nzuri dakika ya 44, baada ya kuokoa mkwaju wa penalti wa beki David Luhende. Penalti hiyo ilitolewa na refa Amon Paul wa Mara baada ya kiungo Awadh Juma kumchezea rafu kwenye eneo la hatari mshambuliaji Ame Ally.  

 Kipindi cha pili, Mtibwa Sugar walicharuka na kuanza kupeleka mashambulizi ya nguvu zaidi langoni mwa Simba SC,Hali hiyo iliwafanya vinara wa hao wa Ligi Kuu wapate bao la kusawazisha dakika ya 58, mfungaji Mussa Hassan Mgosi aliyetumia makosa ya beki wa kulia, William Lucian ‘Gallas’ kuchanganyana na kipa wake, Manyika Jr.
Nalo ba pekee la kiungo Paul Ngway, dakika ya 52 jioni ya leo November 01,2014, limeipa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga SC, Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Yanga SC ilimaliza mchezo huo pungufu, baada ya Nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 80 na refa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, baada ya kumpiga kichwa Rashid Mandawa wa Kagera.
Ngway, mchezaji mkongwe wa timu hiyo ya Wakata Miwa wa Misenyi, Bukoba Vijijini, alifunga bao zuri kwa shuti kali akimalizia krosi ya Julius Kwangwa.

Yanga SC inabaki na pointi zake 10 baada ya mechi sita, ikishinda tatu, sare moja na kufungwa mbili, nyingine na Mtibwa Sugar mjini Morogoro 2-0.


Nalo goli pekee la Jacob Massawe dakika ya 15 limeipa ushindi wa 1-0 Ndanda FC dhidi ya mabingwa watetezi, Azam FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Huo unakuwa mchezo wa pili mfululizo, Azam FC kupoteza baada ya Jumamosi iliyopita kuchapwa 1-0 pia na JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Matokeo hayo, yanaifanya timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Awadh Bakhresa na familia yake ibaki na pointi zake 10, baada ya mechi sita, wakati Ndanda saa inadikisha pointi sita.

Mechi nyingine za ligi hiyo leo November 01,2014, Coastal Union imeilaza 1-0 Ruvu Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga bao pekee la Itubu Imbem dakika ya 54, wakati JKT Ruvu imefungwa 2-1 na Polisi Moro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. 


Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad