HABARI PICHA:-Taswira kutoka eneo la Ajali ya Basi la Simba Mtoto na Fuso ikiua Mtu mmoja October 31,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, November 01, 2014

HABARI PICHA:-Taswira kutoka eneo la Ajali ya Basi la Simba Mtoto na Fuso ikiua Mtu mmoja October 31,2014.

Fuso likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na basi la Simba Mtoto.

Basi la Simba Mtoto baada ya Ajali ambapo Basi hilo lenye namba za usajili T 501 BRZ lililokuwa linasafiri kutoka mkoani Tanga kwenda Dar es Salaam limegongana uso kwa uso na fuso la Mohammed Enterprises lenye namba za usajili T 507 BAE lililokuwa likitokea jijini Dar Jana October 31,2014.

Katika ajali hiyo, dereva wa fuso amepoteza maisha papo hapo huku watu wawili ambao pia walikuwa katika fuso hilo wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu zaidi.

Ajali hiyo imetokea katikati ya Daraja la Mto Wami mkoani Pwani baada ya fuso kufeli breki.

Pichani ni Taswira kutoka eneo la ajali.







Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad