UEFA 2014/2015:-Cheki Picha Welbeck akipiga 3 wakati Arsenal na Real Madrid zikishinda mechi zao October 01,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, October 02, 2014

UEFA 2014/2015:-Cheki Picha Welbeck akipiga 3 wakati Arsenal na Real Madrid zikishinda mechi zao October 01,2014.

Mchezaji  Danny Welbeck akipongezwa na Alexis Sanchez baada ya kupiga hat trick wakati Arsenal ikishinda 4-1 usiku huu wa Oktoba 01,2014 katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 Danny Welbeck amefunga hat trick yake ya kwanza Arsenal ikishinda 4-1 katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Emirates.

Mshambuliaji huyo aliyenunuliwa kutoka Manchester United msimu huu, alifunga mabao hayo katika dakika za 22, 30 na 52 wakati lingine limefungwa na Alexis Sanchez dakika ya 41- huku bao la wageni likifungwa na Burak Yilmaz kwa penalti dakika ya 63.
Kipa wa Arsenal, Szcezesny alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 60 na bado hiyo haikuizuia timu ya Arsene Wenger kushinda.

Mchezo mwingine wa Kundi D, Anderlecht imechapwa 3-0 nyumbani na Borrusia Dortmund kwa mabao ya Ciro Immobile dakika ya 3 na Adrian Ramos dakika ya 69 na 79.

Kundi B, Basel imeichapa 1-0 Liverpool bao pekee la Marco Streller dakika ya 52, wakati Real Madrid imeshinda ugenini mabao 2-1 dhidi ya PFC Ludogorets Razgrad.

Wenyeji walitangulia kupata bao dakika ya sita kupitia kwa Marcelinho kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga kwa penalti mara mbili dakika ya 11 na 25 kuipa ushindi Real Madrid.


Katika Kundi C, Zenit St Petersburg imetoka 0-0 na Monaco huku Bayer Leverkusen ikiitandika 3-1 Benfica, mabao ya Stefan Kiessling dakika ya 25, Heung-Min Son dakika ya 34 na Calhanoglu dakika ya 64, huku Eduardo Salvio akiwafungia Benfica dakika ya 62.

Kundi A bao pekee la Ada Turan limetosha kuipa Atletico Madrid ushindi wa 1-0 dhidi ya Juventus wakati katika mchezo mwingine wa kundi hilo, Malmo FF ya Sweden imeichapa 2-0 Olympiacos ya Ugiriki mabao yake yakitiwa kimiani na M Rosenberg dakika ya 42 na 82.

Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad