UCHAKAVU WA MABASI YA ABIRIA:- Tazama Picha 7 za Basi la Mohamed Trans lililolalamikiwa na Abiria wa Bukoba-Dar. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, October 30, 2014

UCHAKAVU WA MABASI YA ABIRIA:- Tazama Picha 7 za Basi la Mohamed Trans lililolalamikiwa na Abiria wa Bukoba-Dar.

Muonekano wa basi hilo...Ambapo Abiria waliokuwa wakisafiri na basi la Kampuni ya Mohammed Trans  lenye namba za usajili T 774 AWJ kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Bukoba wamelalamikia basi hilo kuwa ni bovu.

Sehemu ya mlango wa abiria wa basi hilo. ................Mmoja wa abiria ambaye hakutaja jina lake alionyeshwa kukerwa na basi hilo akilalamika kuwa mpaka leo asubuhi majira ya saa 1 asubuhi walikuwa bado Kahama wakisubiri basi hilo lilekebishwe tairi.

Mbali na kuwa basi hilo kuonekana kuchoka, pia abiria wamelilalamikia kuwepo kwa kunguni ndani ya basi hilo ambao huwasumbua hasa nyakati za usiku.

Basi hilo kwa mbele. .....Tofauti na abiria hao abiria wengine waliosafiri na basi hilo Alhamisi ya Oktoba 16 kutoka Dar kwenda Bukoba nao walilalamikia huduma za kampuni hiyo wakidai kucheleweshwa katika stendi yao iliyopo eneo la Shekilango jijini Dar.

Abiria hao walidai kuchelewa kuondoka eneo hilo kama ilivyo kawaida muda wa saa 12:00 badala yake waliondoka saa 1:30 asubuhi baada ya kuambiwa kuwa basi lao ambalo ilibidi wasafiri nao lilikuwa na tatizo hivyo kuletewa hilo lenye namba za usajili T 774 AWJ

Abiria hao pia wakilalamika kuumwa na wadudu hao (kunguni) wakati wa safari yao hiyo.

Wasafiri hao wamezitaka mamlaka husika kuchukua hatua kabla basi hilo halijaleta maafa.

(Picha zote na Mdau wa Global WhatsApp 0753 715 779)
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad