Waandamanaji
nchini Burkina Faso leo wamechoma moto bunge la nchi hiyo kupinga kupitishwa
kwa katiba itakayomruhusu rais wa nchi hiyo, Blaise Compaore kuongeza muda wa
kukaa madarakani.
Rais Compaore
anataka kuongeza muda zaidi katika utawala wake wa miaka 27 aliyotumia
kuliongoza taifa hilo.
Taarifa
kutoka Mji Kuu ya nchi hiyo, Ouagadougou, zinasema kuwa ukumbi wa chama tawala
na makao makuu ya chama hicho cha Congress for Democracy and Progress
yamechomwa moto pia.
Bunge hilo
lilitaka kubadili katiba itakayomuwezesha Compaore, aliyeingia madarakani tangu
mwaka 1987 ili aweze kuiongoza tena nchi hiyo mwakani.
Kumekuwepo
kampeni za wapinzani wanaomtaka rais huyo kuachia ngazi na kutogombea katika
uchaguzi wa mwaka ujao.
Kabla ya
kuchomwa moto bunge hilo, polisi walilipua mabomu ya machozi kuwazuia
waandamanaji waliokuwa wakielekea katika jengo la bunge hilo japo takribani
watu 1,500 walifanikiwa kupenya na kulichoma bunge hilo.
Waandamanaji
walionekana wakichoma nyaraka na kupora baadhi ya vifaa vya kompyuta huku
magari yaliyokuwa nje ya jengo hilo nayo yakichomwa moto huku wakisisitiza Rais huyo ajiuzulu mara moja.
|
No comments:
Post a Comment