SOKA WILAYA YA NGARA:-Ngara Stars sasa haoooo Nusu fainali wakiifunga Kabanga FC bao 1-0 baada ya Dk 90. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, October 17, 2014

SOKA WILAYA YA NGARA:-Ngara Stars sasa haoooo Nusu fainali wakiifunga Kabanga FC bao 1-0 baada ya Dk 90.

Timu ya soka ya Ngara Stars imekua timu ya kwanza kufuzu hatua ya Nusu Fainali ya Ligi soka  wilaya ya Ngara mkoani Kagera yenye lengo ya kupata Bingwa wa wilaya 2014/2015,baada ya hii leo October 17,2014  kuifunga timu ya Kabanga FC bao 1-0. 

Mchezo huo uliokuwa mkali kwa kila upande na kuchezwa katika uwanja wa Kokoto mjini Ngara ,Timu zote zilijikuta zikimaliza dakika 90 bila kufungana na ndipo zikaenda dakika 30 za nyongeza ambapo katika dakika 117 ya mchezo,mchezaji Juma Mwanafunzi aliipatia bao Ngara Stars lililowafanya kufuzu hatua hiyo.

Aidha hapo kesho October 18,2014,katika uwanja huo wa Kokoto,Ligi hiyo itaendelea tena katika Robo Fainali ya pili saa 10 jioni kwa kuwakutanisha Walimu FC dhidi ya Benaco Stars huku Jumapili October 19,2014 ,Ngara Boys wakiwa wenyeji wa Rulenge White Stars.
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad