Katika hali ya kustajaabisha
kijana mmoja alietambulika kwa jina moja la Yusuph (Me) mkazi wa Buzebazeba
Ujiji amekutwa amekufa katika korongo la Lebengera jirani na Ofisi za CCM mkoa
katika manispaa ya Kigoma Ujiji huku akiwa amejaa damu katika paji lake la uso
Mara baada ya Jeshi la Polis
kufika eneo la tukio walimpekua marehemu na kumkuta na fedha taslimu kama elfu
tatu hivi na karatasi ambayo haikujulikana maramoja imeandikwa nini.
Tukio hilo limetokea Oktoba 13,2014, eneo tajwa hapo
juu huku umati mkubwa ukiwa umefurika ili kumtambua na kushuhudia tukio hilo.
Katika uchunguzi wa awali
inasemekana tukio hilo limetokea usiku wa siku hiyo,kwani kutwa nzima ya siku
hiyo hapakuonekana mtu ambae amekufa katika eneo hilo.
Mmoja wa wananchi aliekuja
kushuhudia tukio,na ambae ni mfanyakazi katika ofisi moja jirani na eneo la
tukio( jina kapuni) amesema hii imekuwa ni mara ya pili kutokea tukio kama hili
la mtu kukutwa ameuawa na kutupwa katika korongo hili,hivyo anaviomba vyombo
vya usalama kuweka doria ya mara kwa mara eneo hili kwani eneo hili
linakaribiana na Bar pamoja na Ofisi za Hazina Ndogo.
Habari Na:-Dj Sek.
|
No comments:
Post a Comment