NYERERE DAY:- Yaliyojiri wakati CCM wilaya ya Kasulu na Mashabiki wa Michezo Walivyomuenzi Mwalimu Nyerere October 14,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, October 15, 2014

NYERERE DAY:- Yaliyojiri wakati CCM wilaya ya Kasulu na Mashabiki wa Michezo Walivyomuenzi Mwalimu Nyerere October 14,2014.

Katika kuadhimisha miaka 15 ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Chama cha Mapinduzi CCM,wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma,kiliadhimisha kumbukumbu hiyo kwa Bonanza la michezo kwa kuwa na mchezo wa Bao na Soka uliyofanyika jana October 14,2014 mjini Kasulu.

Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Kasulu,Masud Kitowe amesema kwamba  Katika mchezo wa bao,Makundi 12 yalishiliki kwa njia ya mtoano na kubaki makundi 6 ya Robo fainali  yaliyoichuana na kubaki  makundi 3 yaliyocheza hatua ya  mzunguko kutafuta Bingwa.

Katika mchezo huo ,Bingwa alipatikana Gribert Nyambele aka Mwaya Kutoka kundi la (Baba IDD) wa pili  ni Boaz toka kindi la (Sondogo) wa tatu Mussa toka kundi la Deo Lugema. 

ZAWAD:-Kwa kila Mshiriki  walipewa shilingi  5000,wakati Mshindi wa tatu shilingi 30,000 ,wa pili  shilingi 50,000 na Bingwa kuondoka na shilingi  70,000.

Kwenye mchezo wa Soka zilipambana Kasulu United ambaye ni Bingwa wa Kombe la CCM wilaya ya Kasulu 2014/2015 dhidi ya Red Stars waliopambana katika uwanja wa CCM Umoja mjini Kasulu.

Hadi dakika 90 ' mpambano huo haukutoa mshindi na ndipo penati tano tano zilipigwa ,ile piga nipige tayari ilikua giza limeingia   hivyo mechi ika vunjwa bila kupatikana mshindi.

Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kasulu,Masud Kitowe amesema ilibidi kugawa Zawadi ya Jezi seti moja kwa kila timu na Zawadi ya Mpira ilibaki mpaka mechi itakapo rudiwa Mwezi desemba,mwaka huu ndipo itatolewa kwa kuchezwa pambano maalumu la marudiano ambapo MDHAMIN NI MKURUGENZI WA KAMPUNI YA DYOYA CONTRACTOR BW DEVID DYOYA. 



Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad