MAFANIKIO YETU:-Tazama Picha 12 za matukio ya mahafari ya pamoja ya kidato cha 4 na Darasa la 7 katika Shule za Mwilamvya,Kasulu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 26, 2014

MAFANIKIO YETU:-Tazama Picha 12 za matukio ya mahafari ya pamoja ya kidato cha 4 na Darasa la 7 katika Shule za Mwilamvya,Kasulu.


Mkaguzi Mkuu wa Shule Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw.Hadrian Mlelwa akivalishwa scaff na Vijana wa Scout mara baada ya kuwasili Mwilamvya English Medium (Nursery and Primary Schools), ambapo sherehe za mahafari zilifanyika kwenye bwalo la Jenesta Mhagama.

Mkaguzi Mkuu wa Shule Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw.Hadrian Mlelwa, akizindua Mradi wa Maji shuleni hapo ambao umegharimu kiasi cha shilingi milioni 80 ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza tatizo la maji. Chanzo cha maji hayo ni milima ya Heru Wilayani Kasulu,mkoani Kigoma.


Mkaguzi Mkuu wa Shule Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw.Hadrian Mlelwa, akizindua rasmi Jengo la Bwalo la Jenesta Mhagama lililopo Mwilamvya English Medium huku tukio hilo likishuhudiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwilamvya,Bw. Elias Maliyatabu. 

Ujenzi wa bwalo hilo umegharimu shilingi milioni 200.


Mkaguzi Mkuu wa Shule Kanda ya Ziwa Magharibi, Hadrian Mlelwa akiwa katika chumba cha kujifunzia Computer kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwilamvya wilayani Kasulu mkoani Kigoma.


Mgeni rasmi kwenye mahafari hayo Mkaguzi Mkuu wa Shule Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw.Hadrian Mlelwa, akiwa kwenye chumba cha maabara katika Shule ya Sekondari Mwilamvya iliyopo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, ambapo amewasifu Wanafunzi kwa kuonyesha umahiri mkubwa katika masomo ya Sayansi.

Hii ni Maktaba ya Shule ya Sekondari Mwilamvya ambapo Uwiano witabu katika Shule ya Sekondari ya Mwilamvya ni Kitabu kimoja Wanafunzi 2.

Mkaguzi Mkuu wa Shule Kanda ya Ziwa Magharibi,Bw. Hadrian Mlelwa, akitembelea maeneo mbali mbali ya Mwilamvya English Medium huku akisindikizwa na wenyeji wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwilamvya, Bw.Elias Maliyatabu, kulia na Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwilamvya, Bw.Emmanuel Saguda, kushoto.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwilamvya, Bw.Elias Maliyatabu, akiongea kwenye mahafari ya saba ya kidato cha nne Shule ya Sekondari Mwilamvya na mahafari ya kwanza ya darasa la saba Shule ya Msingi Mwilamvya.


Mkaguzi Mkuu wa Shule Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw.Hadrian Mlelwa, akitoa hotuba kwa niaba ya Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi.Jenesta Mhagama, ambaye alikuwa awe mgeni rasmi kwenye mahafari hayo lakini alipata udhuru.


Hawa ndio wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mwilamvya.


Hawa ni wahitimu wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Mwilamvya.

Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad