Papa Francis
amemteua Padre Joseph P. Mlola , wa Shirika la ALCP / OSS kuwa Askofu
mpya wa Jimbo Katoliki Kigoma, Tanzania. Kabla ya uteuzi mpya , alikuwa ni
Gombera wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo Kipalapala, Tabora Tanzania.
Askofu Mteule Joseph P. Mlola, ALCP / OSS, alizaliwa Januari 9, 1966 Mashati
Rombo, Moshi.
Baada ya elimu ya msingi na sekondari, alijiunga na seminari ndogo ya Uru
(Moshi), na baadaye kujiunga Shirika la Utume wa Yesu akiwa katika Seminari Kuu
Kenya, ambako alichukua masomo ya falsafa. Na alikamilisha masomo ya Teolojia
katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo Kipalapala, Tabora.
Alipokea Daraja la Upadre Julai 12, 1997, chini ya maisha ya Jumuiya ya Mapadre
wa Kazi ya Roho Mtakatifu "Opus Spiritus Sancti - ALCP / OSS".
Baada
ya Upadrisho alishika nyadhifa mbalimbali ifuatavyo
1997-1999:Paroko Msaisizi wa Parokia ya Nairagie Enkare, Jimbo la Ngong, Kenya.
1999-2000: Makamu wa Ngombera katika nyumba ya malezi ya Roho Mtakatifu,
Morogoro Tanzania.
2000-2001: Paroko msaidizi Parokia ya Caliti, Avellino, Italia.
2001-2005: Alijiunga katika masomo ya juu ya shahada ya Uzamivu (udaktari),
katika kanuni ya Teolojia, katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana.
2005-2011: Makamu Ngombera katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Charles Lwanga
Segerea, Dar-es-Salaam Tanzania .
Tangu mwaka 2011 hadi uteuzi mpya, alikuwa Gombera wa Seminari Kuu ya Mtakatifu
Paulo Kipalapala, Tabora Tanzania.
Jimbo la Kigoma, liliundwa mwaka 1953,chini ya Jimbo Kuu La Tabora. Lina eneo
la kilomita mraba 45 066 kukiwa na idadi ya watu milioni 2, ambao kati yao 515
701 ni Wakatoliki.
Kuna Parokia 22, , Mapadre 55 ( Mapadre wa Jimbo wakiwa 42
na Mapadre wa Mashirika 13 ), watawa ni 65 na Waseminaristi 19.
Jimbo la Kigoma, imekuwa wazi tangu Juni 27, 2012, kufuatia Askofu wake Protase
Rugambwa, kuteuliwa na Papa mstaafu Benedikto XVI kumteuwa kuwa Askofu mkuu,
Katibu mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu na Rais wa Mshirika
ya Kimissionari ya Kipapa mjini Roma.
|
No comments:
Post a Comment