LIGI KUU VODACOM 2014/2015.-Ni matokeo ya mechi ya Jumamosi October 25,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 26, 2014

LIGI KUU VODACOM 2014/2015.-Ni matokeo ya mechi ya Jumamosi October 25,2014.


Bao la Dakika ya 44 la Samuel Kamuntu limeipa ushindi Ruvu JKT wa Bao 1-0 walipocheza na Mabingwa Azam FC huko Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam na kuwashusha kutoka kileleni.

Kipigo hicho ni cha kwanza kwa Azam FC kwenye Ligi Kuu Vodacom toka Msimu uliopita na kuwafanya waipishe Mtibwa Sugar, ambao wako huko Mbeya Kesho kucheza na Mbeya City, kukaa kileleni.

Huko Kambarage, Shinyanga, Yanga waliichapa Stand United Bao 3-0 kwa Bao za Dakika ya 12 la Geilson Santana "Jaja na Bao mbili za Jerson Tegete, Dakika za 78 na 90.

Tegete aliingizwa Kipindi cha Pili kuchukua Nafasi ya Jaja.

Sasa Yanga wamekamata Nafasi ya 3 wakiwa nyuma ya Vinara Mtibwa Sugar na Azam FC kwa Magoli tu huku Timu zote 3 zikiwa na Pointi 10 kila mmoja.

Huko Sokoine, Mbeya, Simba wameendelea tena na mwendo wao wa Sare baada ya kutoka 1-1 na Prisons na hii ni Sare yao ya 5 mfululizo katika Mechi zao zote za Ligi Msimu huu.

Simba walitangulia kufunga katika Dakika ya 8 kwa Bao la Emmanuel Okwi na Prisons kusawazisha Dakika ya 89 kwa Bao la Hamisi Maingo.

Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
LIGI KUU VODACOM RATIBA.

Jumapili Oktoba 26,2014.

Mbeya City v Mtibwa Sugar [Sokoine, Mbeya]

MSIMAMO LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA 2014/2015.

NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Mtibwa Sugar
4
3
1
0
6
1
5
10
2
Azam FC
5
3
1
1
6
2
4
10
3
Yanga
5
3
1
1
7
4
3
10
4
Coastal Union
5
2
2
1
6
4
0
8
5
JKT Ruvu
5
2
1
2
4
5
-1
7
6
Ruvu Shooting
5
2
1
2
4
5
-1
7
7
Kagera Sugar
5
1
3
1
3
2
1
6
8
Mgambo JKT
5
2
0
3
2
4
-2
6
9
Mbeya City
4
1
2
1
1
0
1
5
10
Tanzania Prisons
5
1
2
2
5
5
0
5
11
Simba
5
0
5
0
5
5
0
5
12
Stand United
5
1
2
2
3
8
-5
5
13
Ndanda FC
5
1
0
4
7
10
-3
3
14
Polisi Moro
5
1
2
2
3
6
-3
3

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad