KUHUSU ‘’RWANDA'S UNTOLD STORY’’Hii ndio Taswira ya Wanyarwanda walivyoandamana kuipinga BBC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, October 24, 2014

KUHUSU ‘’RWANDA'S UNTOLD STORY’’Hii ndio Taswira ya Wanyarwanda walivyoandamana kuipinga BBC.

Hapo Jumatano October 22, 2014, maandamano yalifanyika mjini Kigali dhidi ya BBC kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Prudent Nsengiyumva mjini Kigali.

Katika kikao kilichodumu siku nzima, Wabunge pamoja na Maseneta walijadili kuhusu kipindi hicho,''Rwanda’s Untold Story''

Kilipeperushwa tarehe 1 mwezi huu wa Oktoba na moja ya vituo vya BBC. Wabunge hao walitoa wito wa kusitisha matangazo ya BBC nchini Rwanda.

Wanataka serikali imchukulie hatua mtangazaji wa kipindi hicho, na wale wote waliohusika kutengeza kipindi hicho.
Aidha Bunge nchini Rwanda limepiga kura ya kupiga marufuku BBC nchini humo, kufuatia kipindi maalum cha Televisheni kilichoitwa ''Untold story'' kuhusu mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 kilichopeperushwa na BBC.

Kipindi hicho kilihoji uhusika wa baadhi ya maafisa wakuu serikalini juu ya yale yaliyotokea wakati wa mauaji ya kimbari.

Bunge hilo linataka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya BBC kwa kupeperusha kipindi hicho ambacho wanasema kinahujumu mauaji ya Kimbari na pia kukana mauaji dhidi ya watutsi.
Kipindi hicho kiliwahusisha wataalamu wawili wa Marekani waliohoji maelezo kuhusu mauaji ya kimbare mwaka 1994 ambayo umoja wa Mataifa unasema kuwa watu 800,000 wengi wao watutsi na wahutu wenye msimamo wa kadri waliuawa kinyama.

Habari Na:-BBC Swahili.
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad