KATIBA TANZANIA:-Tazama Picha 4 Yaliyojiri Bungeni baada ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kupiga Kura ya Wazi Leo October 01,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, October 01, 2014

KATIBA TANZANIA:-Tazama Picha 4 Yaliyojiri Bungeni baada ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kupiga Kura ya Wazi Leo October 01,2014.


Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akipiga kura leo Oktoba 01,2014,kwenye ukumbi wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma kupitisha Sura na Ibara za Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.

 Mwanasheria huyo amepiga kura ya wazi na amepiga HAPANA kwa sura na vifungu kadhaa, na vyengine amevikubali.

Baada ya hali kuwa tete Mwanasheria huyo ametokewa kwenye ukumbi wa Bunge kwa mlango maalum chini ya ulinzi.

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar amepiga kura ya wazi na amezikataa ibara kadhaa kama vile 2,9,70 hadi 75,86,128,129,158, 159,160,161,243 hadi 251 na nyongeza ya kwanza ambayo inataja mambo ya Muungano.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Yahya Kassim Issa akiomba mwongozo leo Oktoba 01,2014,Bungeni kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta kuhusu kitendo cha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman kuja kupiga kura na kukataa baadhi ya Ibara za Rasimu ya Katiba inayopendekezwa wakati alijitoa kwenye Kamati ya Uandishi ambapo alitakiwa awepo akitetea maslahi ya Zanzibar, jambo ambalo limewachanganya baadhi ya wajumbe.

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akisindikizwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge Maalum leo mjini Dodoma na Askari Polisi.

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (mwenye Kaunda suti ya kijivu) akisindikizwa kutoka nje ya viwanja vya Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma na Askari Polisi mara baada ya kushutumiwa na baadhi ya Wajumbe wa Zanzibar.

Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad