ZIARA YA MAMBO YA NDANI KASULU:-Waziri Chikawe awaonya Wakimbizi Nyarugusu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 15, 2014

ZIARA YA MAMBO YA NDANI KASULU:-Waziri Chikawe awaonya Wakimbizi Nyarugusu.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiwasalimia watoto wa wakimbizi wakati Waziri huyo alipokuwa anatembelea baadhi ya familia za wakimbizi hao kwa lengo la kuwasalimia pamoja na kuangalia jinsi maisha yao wanavyoyaendesha kambini hapo Septemba 12,2014.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe amewataka wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu kuacha tabia ya kuwaozesha watoto wenye umri mdogo kwa kuwa ni kuwiangiza katika matatizo wakati wa kujifungua.

Akizungumza na mamia ya wakimbizi hao wilayani Kasulu Kigoma, Waziri Chikawe alisema katika maisha yake ni mpambanaji wa kupinga ndoa za utotoni zinazowaletea athari watoto.

Wapeni haki zao watoto wenu, utamaduni wa kuwaozesha watoto wadogo sio mzuri achani na muulaani kwani mkifanya hivyo mtawaletea matatizo makubwa watoto wenu hasa wakati wa kujifungua,” alisema Chikawe.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole aliwaonya wakimbizi hao kuacha tabia ya kuwaoza watoto wao kwani kufanya hivyo wakimbizi watashindwa kupata fursa ya kwenda Marekani.

Si mnajua tunawaandaa kwenda Marekani? Kama mnalijua hilo basi endapo mkimbizi atampa mimba mtoto mdogo, basi hapati nafasi ya kwenda Marekani hivyo kuweni makini,” alisema Joyce.

Wakimbizi 30,000 wa kambi ya Nyarugusu wanatarajia kuhamishiwa Marekani kuanzia mwaka 2015.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad