Mzimu wa
posho umeibuka upya katika Bunge la Katiba, safari hii wajumbe wake wa Kamati
ya Uandishi wakiomba walipwe posho maalumu ya Sh500,000 kwa siku kutokana na
kazi ya kuandika Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.
Habari
zilizolifikia Mwananchi na kuthibitishwa na uongozi wa Bunge zinasema kuwa
tayari maoni ya wajumbe yamewasilishwa kwa uongozi kwa ajili ya uamuzi.
Wajumbe wa
kamati hiyo kwa sasa wanalipwa posho maalumu ya Sh210,000 zaidi kwa siku, nje
ya ile ya Sh300,000 kwa siku wanayolipwa wajumbe wote wa Bunge hilo.
Kamati hiyo
inayoongozwa na Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi-CCM
inahusisha baadhi ya vigogo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Serikali
ya Jamhuri ya Muungano.
Vigogo hao
ni pamoja Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Asha-Rose Migiro, Mwanasheria Mkuu
Jaji Frederick Werema, Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Othman Masoud Othman
aliyejiuzulu ujumbe wa kamati hiyo hivi karibuni kwa sababu ambazo
hazijaelezwa.
Katibu wa
Bunge, Yahaya Khamis Hamad pamoja na kukiri kuwa kamati hiyo imeomba kuongezwa
kiasi hicho cha posho, alisema Kamati ya Uongozi ambayo ndiyo huamua,
haijayajadili maombi hayo na kuyatolea uamuzi.
Chenge
hakupatikana jana kuzungumzia maombi hayo.
Gharama
kuongezeka.
Endapo
Kamati ya Uongozi inayoongozwa na Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta itaridhia
maombi hayo kwa wajumbe 24 wa kamati hiyo, Bunge hilo litatumia Sh12 milioni
kwa siku.
Vyanzo vya
habari vimedokeza kuwa iwapo nyongeza hiyo itaanza kulipwa, wajumbe wa kamati
hiyo watakuwa wakizoa jumla ya Sh800,000 kwa siku.
“Msingi wa
kuomba posho hiyo ya Sh500,000 kwa siku unatokana na wajumbe wa kamati kufanya
kazi hadi usiku wa manane,” alidokeza mmoja wa wajumbe wa Bunge.
“Unajua kuna
‘presha’ kubwa kwamba Rasimu ya Katiba inayopendekezwa iwe imetoka Septemba 21,
sasa hiyo inaifanya kamati hiyo kufanya kazi hadi usiku,” alifafanua mjumbe
huyo.
Kwa sasa
kamati hiyo imekuwa ikifanya kazi ya ziada kuingiza michango ya wajumbe wa
Bunge hilo inayotokana na majadiliano baada ya kamati kumaliza kuwasilisha
taarifa zake Septemba 8, mwaka huu.
Kamati hiyo
inatarajiwa kuendelea na mchakamchaka huo hadi hatua ya Rasimu ya Katiba
inayopendekezwa itakapopigiwa kura na wajumbe wa Bunge hilo kuanzia Septemba
26, mwaka huu.
Katibu
aitetea
Katibu wa
Bunge, Hamad aliitetea kamati hiyo akitaka Watanzania kufahamu kuwa wajumbe
wake wamekuwa wakifanya kazi kubwa na wamekuwa wakitoka katika vikao saa 8.00
usiku.
“Hata jana
(Jumamosi) mimi nilitoka pale saa 5.00 usiku niliwaacha ndiyo wanaletewa
chakula cha usiku,” alisema Hamad.
Alisema hata
baada ya wajumbe kukamilisha kazi yao, watendaji wamekuwa wakikesha ili
kukamilisha kazi walizopewa na kamati hiyo.
Wakati Bunge
hilo lilipoanza vikao Februari mwaka huu, baadhi ya wajumbe walitaka posho ya
Sh300,000 wanayolipwa iongezwe wakisema ilikuwa haitoshelezi kuishi mjini hapa
na kudai .
Habari na
:-Mwananchi.
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
|
Monday, September 15, 2014
SOMA HII KUTOKA GAZETI LA MWANANCHI:- Wataka posho ya Sh500,000 kwa siku..??
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment