UNYAMA:-Waliokufa kwa moto Geita wafikia wanne..’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 16, 2014

UNYAMA:-Waliokufa kwa moto Geita wafikia wanne..’

Idadi ya watoto wa familia moja waliokufa kwa ajali ya moto katika nyumba ya wazazi wao waliyokuwa wakiishi, mkoani Geita, imeongezeka kutoka watatu hadi wanne, baada ya mmoja wao aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando, mkoani Mwanza, kufariki dunia.
Mtoto huyo, Scolastika (15), ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Mwatulole, alizikwa Septemba 14,2014.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Kitongoji cha Elimu, Kata ya Kiangalala, mjini Geita, mara baada ya kumzika mtoto wake wa nne, alisema ‘tulikiona kifo’.

Alisema alimwambia mkewe, Angelina Gasper, wapige magoti na kuomba nusura ya Mungu baada ya moto huo kuzuka katika nyumba wanayoishi.

Nyumba hiyo iliteketezwa usiku wa Septemba 7, mwaka huu, baada ya watu wasiofahamika kuimwagia mafuta ya petroli.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie.

Watoto wengine waliotetekea katika ajali ya moto huo, ni Reginald Robert (9), ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne na Sofia (6) wa Shule ya Msingi Ukombozi na Remijius (4) wa Chekechea, walifariki papo hapo.

Mkewe, Angelina akizungumza kwa shida kutokana na kuondokewa na watoto wake wanne, alisema huo si msiba zaidi ya msiba, kutokana na kubakiwa na watoto wawili kati ya sita, ambao wanne wakifariki katika tukio hilo.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya, Dk. Adam Sijaona, alisema kuwapo kwa tukio hilo kumemfanya akutane na mkasa, ambao hajawahi kukutana nao.

Afisa Mtendaji kata ya Kalangalala, Hamad Hussein, alisema waliotenda tukio hilo walimimina mafuta ya petroli milangoni na madirishani na kuilipua nyumba hiyo iliyoezekwa kwa bati inawezekana kwa chuki binafsi ama migogoro ya ardhi.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Hassan Mcharo na Afisa Mtendaji wa Mtaa huo, Simfukwe Ally, kwa pamoja wamelaani tukio hilo wakati wakizungumza na gazeti hili juzi.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie, akizungumza kwa masitikiko kuhusu tukio hilo, alisema amesikitishwa na kitendo hicho na kuagiza kuhakikisha kuanzia ngazi ya mtaa hadi wilaya wanashirikiana kuhakikisha waliohusika na unyama huo wanakamatwa.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad