BUNGE LA KATIBA TANZANIA NI HASARA:-Mabilioni yake yangetosha kujenga zahanati 600…Pia Noti zikipangwa barabarani ni Dar hadi Bukoba. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 16, 2014

BUNGE LA KATIBA TANZANIA NI HASARA:-Mabilioni yake yangetosha kujenga zahanati 600…Pia Noti zikipangwa barabarani ni Dar hadi Bukoba.


Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Prof. Mark Mwandosya ameeleza kuwa mpaka ifikapo mwaka 2055 Tanzania itakuwa imeachana na umaskini katika nchi ya uchumi wa kwanza endapo kutakuwa na dhamira ya dhati hususani kuwa kuandika Katiba yenye kuleta nafuu kwa watanzania kwani kila kitu kwa Waafrika kinawezekana pasipo kuwa na Wazungu.

 Taifa linaelekea kupata hasara kubwa ya zaidi ya Sh. bilioni 120 baada ya kushindwa kupatikana kwa katiba mpya kama ilivyokusudiwa.

Kiasi hicho cha fedha zitakazopotea bure kinatokana na makadirio ya jumla ya fedha zitakazojumuisha mchakato wote uloiodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, ukianzia wakati wa kuundwa kwa Tume Maalum ya Mabadiliko ya Katiba na pia kuwapo kwa vikao vya Bunge Maalum la Katiba vinavyoendeloea mjini Dodoma na kutarajiwa kusitishwa Oktoba 4 mwaka huu.

Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE na kuwahusisha wachambuzi mbalimbali wa masuala ya siasa na uchumi umebaini kuwa kwa kukadiria, ikiwa wajumbe wote waliopo bungeni hivi sasa watakuwa wakihudhuria kila kikao katika ngwe ya pili iliyoanza Agosti 5, maana yake ni kwamba kila mmoja ataondoka na Sh. milioni 12.9 za posho za siku 43 za kazi pamoja na fedha nyingine kiasi cha Sh. 4,140,000 zitakazotokana na posho watakayoipata katika siku 18 zisizokuwa za kazi.

Inaelezwa kuwa wajumbe hao hulipwa posho ya Sh. 300,000 kila mmoja katika siku za kazi wanazohudhuria kikao huku wanapokosa kikao kwa ruhusa maalum, pamoja na siku zisizokuwa za kazi hupokea posho ya Sh.230,000.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Hamad Rashid amewaomba viongozi  kuheshimu na kutii sheria.

Hadi sasa, wajumbe waliojisajili baada ya kuanza kwa ngwe ya pili wanakadiriwa kuwa 528, idadi ambayo haihusishi wajumbe 101 wakiwamo wanaotoka katika kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao walisusia vikao hivyo tangu April 16, 2014 wakipinga kubadilishwa kwa rasimu iliyowasilishwa na Tume iliyoongozwa na Warioba kutokana maoni yaliyokusanywa kutoka kwa wananchi.

Inaelezwa kuwa kwa hesabu hizo, jumla ya kiasi cha fedha kitakachotumika tangu kuanza tena kwa Bunge hilo Agosti 5 hadi Oktoba 4 kitapanda zaidi kwani hadi kusitishwa kwa bunge hilo katika awamu hii ya pili, kila mmoja atakayehudhuria bila kukosa atapokea jumla ya Sh. 17,040,000.

Hadi kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita hakukuwa na takwimu rasmi kutoka ofisi ya Bunge Maalum la Katiba kuhusiana na idadi ya wajumbe waliopo kwenye bunge hilo linaloendelea mjini Dodoma.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

GONGA HAPA KUSOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad