UJIRANI MWEMA:-Hiki ndicho kikosi cha Ngara Stars kilichoikung’uta 3-0 Timu ya Lieverenwari kutoka Mkoa wa Chankuzo nchini Burundi Septemba 20,2014 mjini Ngara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 21, 2014

UJIRANI MWEMA:-Hiki ndicho kikosi cha Ngara Stars kilichoikung’uta 3-0 Timu ya Lieverenwari kutoka Mkoa wa Chankuzo nchini Burundi Septemba 20,2014 mjini Ngara.


Ni kikosi cha Timu ya  Ngara Stars  jana Jumamosi Septemba 20,2014,katika Picha yao ya Pamoja ambapo kimetakata vyema katika dimba lake la nyumbani la kokoto mjini Ngara baada ya kucheza soka safi na la kuvutia na hatimaye kutamba   kwenye uwanja  wao  huo  dhidi ya  timu ya mkoa wa Chankuzo kutoka nchini Burundi,timu ya Lieverenwari.


Kikosi cha Timu ya Mkoa wa Chankuzo nchini Burundi Lieverenwari katika picha ya pamoja uwanja wa Kokoto mjini Ngara.

 Mechi hiyo  ilikuwa ya kirafiki ya kimataifa ,ilikuwa na lengo la kukuza na kudumisha ujirani mwema baina ya wilaya ya ngara mkoani kagera nchini Tanzania na mkoa wa Chankuzo uliopop nchini Burundi na wageni kushitushwa kwa kipigo cha bao 3-0.

Mgeni rasmi katika pambano hilo,Katibu Tawala wilaya ya Ngara Vedastus Tibaijuka akizikagua na kusalimiana na wachezaji wa Ngara Stars kabla ya mchezo kuanza.

Katika mchezo huo goli za Ngara Stars zilifungwa na Edward Kijanjali  dk ya 19 , 25 na dk ya  ya  40 likifungwa na Fadhiri Rashid.

Aidha Ngara Stars leo Septemba 21,2014 ,majira ya jioni wanashuka tena uwanja wa Kokoto kucheza mchezo wa Kirafiki wa Ujirani Mwema na Bingwa wa Kombe la Chama cha Mapinduzi CCM 2013/2014,Timu ya Kasulu United.

Kasulu United iko hapa wilayani Ngara katika ziara yake ya kimichezo ya siku mbili ambapo Jana Septemba 20,2014,ilicheza na rulenge White Stars mjini Rulenge na kuwafunga bao 2-0.
 UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad