NAJUA WAJUA ILA HII ZAIDI:- Unazijua kesi zilizowahi kuwatesa wakali hawa wa Bongo ? - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 21, 2014

NAJUA WAJUA ILA HII ZAIDI:- Unazijua kesi zilizowahi kuwatesa wakali hawa wa Bongo ?

Diamond Platnumz-Nasib Abdul.

 Haikuwa tofauti sana na ile ya Chris Brown inayomfanya azidi kukaa rumande bila dhamana hadi hii leo, hii ya Diamond naye ilikuja baada ya kufikishwa mahakama ya Bomani mjini Iringa baada ya kumshambulia na kumvunjia vyombo vya kazi mwandishi wa habari, ikiwemo camera na vingine.

 Mwanasheria wa mwandishi huyo alitoa tamko na kumpa Diamond siku 21 awe amelipa sh milion 30 la sivyo atafikishwa Mahakamani.

Awali diamond alifikishwa mahakamani, na mahakama iliamuru alipe Tsh 50,000 au kifungo cha miezi  sita jela.

Mwandishi huyo wa habari alisema asingemfikisha DIAMOND mahakamani kama angekubali kumuomba msamaha, lakini kwa sababu hakukubali kufanya hivyo ndio maana akaamua kumfungulia kesi.
Wema Sepetu.

Wema aliburuzwa mahakamani kwa shtaka lilokuwa linamkabili la kudaiwa kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga vibao Meneja wa Hoteli, Goodluck Kuyumbu,ingawa baada ya Wema kupandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake ya kudaiwa kufanya vurugu, kushambulia kwa kumpiga makofi na kumtukana Kayumbu, mbele ya hakimu, Wema alikana mashitaka hayo.

Mwaka 2009, Wema alidakwa na Polisi Kituo cha Magomeni na baadaye kupandishwa katika Mahakama ya Kinondoni, Dar kwa Hakimu Emilius Mchalu kwa kosa la kuvunja kioo cha gari la aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, Marehemu Steven Kanumba chenye thamani ya shilingi milioni moja. Hata hivyo, Kanumba aliifuta kesi hiyo.
Kajala Masanja.

Kajala alijikuta yupo ndani ya mikono ya sheria ndani ya mahakama kwa kosa lilokuwa linamkabili yeye mwenyewe na aliyekuwa mume wake ajulikanaye kama Faraja Chambo , katika kesi iliyokuwa inamkabili ya kuuza nyumba iliyopatikana kwa njia ya rushwa na kuwekewa kizuizi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ,ingawa kajala ndiye aliyekuwa anadai hakuwa na taarifa yeyote ya upatikanaji wa nyumba hiyo, hata hivyo mahakama ilishia kumshitaki kifungo cha miaka au kulipa faini ya shilingi milioni 13, jambo ambalo rafiki yake mkubwa Wema Sepetu ambapo ndiye aliyeweza kufanikisha kumtoa best yake huyo kwa kulipa faini yote ya milioni 13 na Kajala kuachiwa huru.
Lulu Michael.

Akiwa bado na umri mdogo msanii Lulu alifikishwa mahakamani kwa kosa la kumuua msanii mwenzie bila kukusudia ambaye inasemekana alikuwa mpenzi wake, Kesi hiyo ilimgharimu  kukaa rumande kwa miezi mingi tu kwa sababu kushtakiwa kwa kosa la kuua halina dhamana..ila baada ya purukushani za mahakamani kutetea ukweli,mwisho wa siku ukweli halisi kugundulika, na aliweza kuachiwa huru mara moja. 

Luu Michael ndiye msanii pekee aliyetokea kupitia mkasa huo akiwa bado kwenye umri mdogo
 UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad