Bidhaa mbalimbali za madukani zikiwa tayari
kwaaajili ya kuteketezwa baada ya muda wake wa matumizi kuisha,kufuatia msako
wa kushitukiza wa TFDA.
Na Editha Karlo - Kigoma
Zaidi ya
Tani 24 za vyakula,dawa za binaadam na vipodozi zimeteketezwa na mamlaka ya
chakula na dawa(TFDA)katika mikoa minne ya kanda ya katikwasababu ya kutofaa
kwa matumizi ya binaadam.
Akizungumza
wakati wa zoezi la uteketezaji wa bidhaa hizo zilizokamatwa katika zoezi la
kustukiza ndani ya Manispaa ya Kigoma ujiji Mkoani Kigoma, Mkaguzi wa TFDA kanda
ya kati Bw.Engliber Bilashoboka alisema kuwa bidhaa hizo zilikamatwa kati ya Julai
mwaka jana (2013 ) na Juni mwaka huu (2014).
Bw. Bilashoka
alisema kuwa kuteketezwa kwa bidhaa hizo kunatokana na ukaguzi unaofanywa na
maofisa wa TFDA katika mikoa mbalimbali nchini na lengo likiwa ni kuondoa
sokoni bidhaa zilizoisha muda wake na zisizofaa kwa matumizi ya bindaadam
Alisema
pia kufuatia zoezi hilo mamlaka yake imekifungia kiwanda cha mikate cha Kigoma
bekari baada ya kukutwa na tani 1.5 za mikate mibovu, pamoja na machinjio ya
ujiji kwa kufanya shughuli zake katika hali inayotishia afya za wananchi
Alisema
bidhaa hizo zimekamatwa katika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na dodoma alisema
kuwa katika bidhaa zilikamatwa na kuteketezwa nyingi zilikuwa zikiuzwa huku
muda wake wa kuwa sokoni ukiwa umeisha na zingine zimepigwa marufuku kuuzwa
nchini.
Ofisa huyo alisema kuwa uteketezaji katika manispaa ya kigoma kwa muda wa wiki
moja mpaka sasa ,alisema mamlaka ya ke imeteketeza zaidi ya tani 4.1zenye
thamani ya shilingi milioni 24 ambavyo havifai kwa matumizi ya binaadamu
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Moses Welansari akizungumzia
zoezi hilo alisema kuwa wamekuwa wakikutana changamoto za wenye maduka
zilizokatazwa au zilizoisha muda wake wa matumizi.
''Elimu
imekuwa ikitolewa kwa wafanyabiasha mara kwa mara ili kuepuka kuweka sokoni
bidhaa zisizotakiwa na mamlaka za serikali na zilizoisha muda wake ''alisema
Kaimu Mkurugenzi
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
|
No comments:
Post a Comment