UHURU WA DEMOKRASIA:-Tazama Picha 7 za Jinsi Raia wa Scotland walivyopokea Matokeo ya mwisho baada ya kupiga kura ya kutaka kuwa taifa hur Septemba 19, 2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 20, 2014

UHURU WA DEMOKRASIA:-Tazama Picha 7 za Jinsi Raia wa Scotland walivyopokea Matokeo ya mwisho baada ya kupiga kura ya kutaka kuwa taifa hur Septemba 19, 2014.

Wananchi wa Scotland waliokuwa wakitaka kujitenga na Uingereza wakiangua kilio huku walioshinda wakiwa na furaha baada ya matokeo kutangazwa.

 Matokeo ya kura za maoni nchini Scotland yametoka, kura 1,914, 187 sawa na 55% walipendelea kuendelea kuwa sehemu ya Uingereza ikilinganishwa na kura 1,539,920 sawa na 45%  ambao walipiga kura ya kutaka kuwa Taifa huru linalojitawala lenyewe . 
Muungano wa miaka 307 baina ya nchi hiyo na Uingereza katika kura ya maoni ya kihistoria iliyokuwa ikisubiriwa kuamua iwapo Scotland itajitenga,huko Glascow, mji mkubwa kabisa wa Scotland asilimia 61 ya wapiga kura walichagua “Ndio” kuunga mkono umoja uliopo kuendelea kuwa hai na asilimia 39 walipiga kura kuupinga umoja huo. 

Hata hivyo wapiga kura katika mji mkuu wa Scotland, Edinburgh na Aberdeen mji wa tatu kwa ukubwa nchini humo ulikataa kuwa taifa linalojitawala lenyewe kwa wingi mkubwa wa kura.

“Watu wa Scotland wamezungumza. Tumechagua umoja dhidi ya mgawanyiko na mabadiliko chanya kuliko mgawanyiko usio na maana”.



Katika hotuba inayoelezea kushindwa kwake, kiongozi wa kitaifa wa Scotland, Alex Salmond pichani, aliita kura ya maoni tathmini ya utaratibu wa kidemokrasia na aliwasihi wafuasi wanaotaka Scotland kujitenga kukubali matokeo ya kura.

“Watu wengi wa Scotland wameamua kupiga kura ya hapana kwa kipindi hiki, kutokuwa taifa huru. Ninakubali matakwa hayo ya watu na ninatoa mwito kwa wa-Scotland wote kufuata sheria katika kukubali matakwa ya demokrasia ya watu wa Scotland”.



Wananchi walipiga kura kwenye vituo 2,600 vya kupiga kura vilivyokuwa nchi nzima kwa kuchagua neno “Ndio” au “Hapana” kwenye swali la kura ya maoni linalouliza kwamba “Ni vyema Scotland iwe taifa huru?”.

Upande uliopinga kujitenga kwa umoja huo unasihi kwamba kura ya “Ndio” itaharibu uchumi wa Scotland na kuvuruga maisha ya kila mtu kama ushirika wa Uingereza ulioundwa mwaka 1707 unavunjika.  
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad