UEFA 2014/2015:-Kilichowakuta Arsenal v/s Dortmund kwenye Champions League na Matokeo mengine hiki hapa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 17, 2014

UEFA 2014/2015:-Kilichowakuta Arsenal v/s Dortmund kwenye Champions League na Matokeo mengine hiki hapa.

Mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck alipata nafasi nzuri ya kufunga hapa bao ambalo lingekuwa la kuongoza kwa Arsenal, lakini akakosa mpira ukimpita namna hii.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

Katika mchezo wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wa ulaya UEFA 2014/2015,Jana September 16,2014, Arsenal  wakicheza Ugenini huko Jijini Dortmund Uwanjani Signal Iduna Park, wameanza vibaya Mechi za Kundi D la UEFA  baada kupigwa Bao 2-0 na Borussia Dortmund.

Hadi Mapumziko Arsenal walikuwa nyuma kwa Bao 1-0 kwa Bao safi sana na la kifundi la Mtaliana Ciro Immobile aliekokota Mpira toka nusu yake ya Uwanja na kuihadaa ngome ya Arsenal kina Koscielny na Gibbs na kukutana uso kwa uso na Kipa Szczesny aliedanganywa na Mpira kupita Kulia kwake na kutinga wavuni katika Dakika ya 44.
Dakika ya 47 ya Kipindi cha Pili, Pierre-Emerick Aubameyang aliipa Dortmund Bao la Pili baada ya bonge la Pasi kutoka kwa Kevin Großkreutz kufuatia kaunta ataki murua.

Hadi mwishoni Dortmund 2 Arsenal 0.
Nao Mabingwa Watetezi wa Ulaya, Real Madrid, wakiwa kwao Santiago Bernabeu wameanza utetezi wa Taji lao vyema kwa kuitandika FC Basel ya Uswisi Bao 5-1 katika Mechi ya kwanza ya Kundi B.

Real Madrid waliongoza 4-1 kufikia Haftaimu kwa Bao za Suchy aliejifunga mwenyewe Dakika ya 14, Gareth Bale, 30, Ronaldo, 31, na James Rodriguez, 36 huku FC Basel wakifunga Bao lao Dakika ya 38 kupitia Gonzalez.

Kipindi cha Pili, Dakika ya 79, Karim Benzema alifunga Bao la 5 kwa Mabingwa wa Ulaya Real Madrid.

Hadi mwisho Real 5 FC Basel 1.

Penati ya Dakika za Majeruhi ya Steven Gerrard iliwapa Liverpool ushindi wa Bao 2-1 walipocheza na Ludogorets Razgrad ya Bulgaria katika Mechi ya kwanza ya Kundi B ,kwenye Uwanjani Anfield.

Straika mpya, Mario Balotelli, aliwapa Liverpool uongozii wa Bao 1-0  katika Dakika ya 82, hilo likiwa ni Bao la kwanza kwa Balotelli kwa Klabu yake, lakini Dakika ya 90 Wachezaji wawili waliotokea Benchi, Younes Hamza na Dani Abalo walishirikiana vyema na Abalo kusawazisha.

Penati iliyozaa Bao la ushindi ilitokea baada Kipa Borjan kudaiwa kumwangusha Borini.

Hadi mwisho Liverpool 2 Ludogorets Razgrad 1.

MAKUNDI UEFA 2014/2015-MATOKEO.

Jumanne Septemba 16,2014.

KUNDI A

Juvsentus 2 – 0 Malmö FF 

Olympiakos 3 – 2  Atlético Madrid 

KUNDI B 

Liverpool 2 – 1  Ludogorets Razgrad 

Real Madrid 5 – 1  FC Basel 

KUNDI C 

Benfica 0 – 2 Zenit St Petersburg 

Monaco 1 – 0 Bayer 04 Levserkusen 

KUNDI D 

Borussia Dortmund 2 – 0 Arsenal 

Galatasaray 1 – 1 RSC Anderlecht 

UEFA 2014/2015 RATIBA YA MAKUNDI

Jumatano Septemba 17,2014.

**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku

KUNDI E 

Bayern Munich VS Man City

AS Roma VS CSKA Moscow

KUNDI F 

Ajax VS Paris St-Germain

Barcelona VS APOEL Nicosia

KUNDI G 

Chelsea VS FC Schalke 04

NK Maribor VS Sporting Lisbon

KUNDI H

Athletic Bilbao VS Shakhtar Donetsk

FC Porto VS BATE Borisovs

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad