UCHAGUZI MKUU CHADEMA:-Soma Yaliyojiri Leo Septemba 14,2014 katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 14, 2014

UCHAGUZI MKUU CHADEMA:-Soma Yaliyojiri Leo Septemba 14,2014 katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.




Wajumbe wa Chadema wakiwa ndani ya Ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya uchaguzi mkuu. 

 Katibu mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa anasoma taarifa kuwa CHADEMA inao wajumbe 1049 na hadi taarifa inasomwa ukumbini wamekwisha jisajiri wajumbe 922 hivyo kwa mjibu wa katiba huo ni mkutano halali katika akidi.

 (Picha zote na Chadema)

Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa kumpata mwenyekiti na makamu wenyeviti wake watakaokiongoza chama hicho kwa miaka mitano umeanza katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam leo Septemba 14,2014.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe katika hotuba yake,ameanza kwa kuwakumbuka viongozi na wanachama wote waliouawa ama kufa kwa sababu mbalimbali.

Amewapongeza wajumbe wote waliochaguliwa mikoani na kuwataka kulinda imani hiyo.Anawapongeza pia viongozi wote kote nchini na watumishi wa makao makuu ambao utumishi wao unakoma leo Septemba 14,2014,rasmi.

Kamanda Mbowe anawatambulisha rasmi viongozi wa mabaraza ya CHADEMA waliochaguliwa akiwemo Mwenyekiti wa Bawacha Halima Mdee na Katibu wake Grace Tendega,Viongozi wa Bavicha Pascal Patrobass na Katibu wake Julius Mwita na pia amewatambulisha viongozi wa wazee.

Kamanda Mbowe anaeleza kwa kirefu kuhusu historia ya chama.Anaeleza wapi chama kimetoka mpaka leo.Anawataja waasisi na viongozi wote wa chama kwa awamu zote na anasema katika waasisi wa chama 36 waliobaki hai mpaka sasa hawazidi 5.

Kamanda Freeman Mbowe ametuma salaam kwa mamluki na vibaraka wote waliodhani wanaweza kuvuruga CHADEMA.

Anawaambia rasmi kwamba leo anamaliza muda wake wa uongozi chama kikiwa salama kabisa.

Anasema kamwe hakuna mtu maarufu ndani ya CHADEMA na hakuna kibaraka yeyote atakayevumiliwa kuvuruga chama hiki.

Mbowe anasema chama kitaanza utaratibu rasmi wa kukagua utendaji wa viongozi kwa ngazi zote kote nchini na kiongozi ambaye atashindwa kutimiza malengo yanayotarajiwa atang'olewa madarakani.

Kamanda Freeman Mbowe anatoa sasa rasmi kauli ya chama kuhusu Uhuni na Ubatili wa bunge la katiba unaoendelea huko Dodoma.

Mbowe anasema kinachoendelea Dodoma ni wizi,ubadhirifu na utapeli wa mali za umma.Anamlaani Samwel Sitta anayejifanya ndiye Rais wa nchi hii na kutapanya pesa za nchi hii kwa kadiri apendavyo bila kunyooshewa kidole na yeyote.

Mwenyekiti Mbowe ameutaka mkutano mkuu uazimie rasmi bunge batili la Katiba livunjwe mara moja.

Endapo kama hilo halitafanyika uitishwe mgomo wa kitaifa kwa sekta zote na maandamano kote nchini yasiyokoma.Wajumbe wote wanasimama na kushangilia kwa shangwe kuu kuunga mkono tamko na kauli hiyo kama maazimio.

Pia Mkutano mkuu huu umeazimia wanasheria wote waangalie namna ya kufungua mashtaka kote nchini kupinga mchakato huu haramu kule Dodoma.

Mkutano mkuu pia umeazimia viongozi wote wa chama majimboni waende waandae taratibu za namna ya kushiriki migomo na maanadamano kupinga bunge haramu la Katiba.

Pia chama kikae na wenzetu wa UKAWA kukubaliana namna nyingine za kupambana na wizi na ubadhirifu unaoendelea Dodoma.

Kamanda Freeman Mbowe anawashukuru wajumbe wote wa mkutano mkuu na kutangaza rasmi kuvunja uongozi wote wa kitaifa uliokuwepo kutokana na kumaliza muda wake kikatiba.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad