UCHAGUZI MKUU CHADEMA:-Hii ndio orodha ya Wanachama waliojitokeza Kugombea Nafasi Mbalimbali za Taifa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 04, 2014

UCHAGUZI MKUU CHADEMA:-Hii ndio orodha ya Wanachama waliojitokeza Kugombea Nafasi Mbalimbali za Taifa.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa orodha ya wanachama wake waliojitosa kugombea nafasi mbalimbali za taifa katika mabaraza huku mnyukano mkali ukiwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu mkuu, Naibu katibu mkuu na Uenezi.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Septemba 03,2014, Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uratibu wa Kanda, Bw.Benson Kigaila, alisema katika Baraza la Vijana, Wanawake na Wazee, nafasi hizo zimepata wagombea zaidi ya watano.

Kigaila, alisema kwa upande wa Baraza la Wanawake (Bawacha), wanachama sita wamejitokeza kuwania Uenyekiti akiwamo Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Lilian Wassira, Sophia Mwakagenda, Rebeca Magwisha, Diwani wa Kunduchi, Janet Rite na Mbunge wa viti maalum, Chiku Abwao.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bawacha Bara (1), na Visiwani (1), waliogombea wako sita ambao ni Sina Manzi, Victoria Tindabatangile na Hawa Mwaifunga wakati kwa upande wa Zanzibar ni Hamida Abdalah, Nasra Jusha Barwan na Mbunge wa Viti maalum, Mariamu Salum Msabaha anayetetea nafasi hiyo.

Kwa upande wa Katibu Mkuu Bawacha waliogombea wako sita, Catherine Vernand, Grace Tendega, Anna Mughwira, Nagy Kaboyoka, Mbunge Viti maalum Paulina Gekul na Mbunge Viti maalum, Naomi Kaihula anayetetea nafasi hiyo.

Waliogombea nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara (1), na Visiwani (1) wako watano ambao ni Clara Mayuki na Yudith Mchaki wa Visiwani wakati Bara ni Ester Daffi, Florence Makazigwa na Kunti Majala.

Katika Baraza la Vijana la CHADEMA (Bavicha), walijitokeza nafasi ya mwenyekiti wako 13, ambao ni Daniel Naftal, Upendo Peneza, Pachal Patrobas, Ephata Nanyaro, Freddy Hatari, Filipo Mwakitinge, Mruta Masolwa, Godfrey Bagamba, Meshack Michael, Lazoro Kapinga, Mussa Mabawa, Alex Thomas na Joseph Mashinga.

Waliogombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bavicha Taifa Bara nafasi (1), na Visiwani (1), wako 15 akiwamo Johnson Luzibukya, Aggrey Dud, Ibrahim Bashe, Khalid Ausi, Julieth Lushuli, Nusrtat Hanje, Jane Nyamsenda, Jesca Kishoa, Rose Mayemba, Zainab Ashraff, Patrick Kpura, Sharif Suleman Hamis, Francis Werema, Zendi Marano Abdulahi na Shaban Omary Shaban.

Nafasi ya Katibu Mkuu wa Bavicha Taifa imegombewa na wanachama 10 ambao ni Fahamu Juma, Alphonce Mwamwile, Goodluck Moreli, Paulo Makuli, General Kaduma, Benson Mramba, Methew Kishili, Meo Benard, Salim Mpanda na Julius Mwita.

Kwa upande wa nafasi ya Uhamasishaji/Uenezi wa Bavicha Taifa waliojitokeza ni Julius Kapunda, Daniel Sanga, Musaa Ndile, Edward Simbeye, Moses Mwaifunga, John Lutulagala, Francis Marwa, Pina Baharia, Baraka Mfilinge, Amina Saguti, Justine Simon na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassary.

Baraza la Wazee waliojitokeza kugombea nafasi ya Mwenyekiti ni Kayaga Ismale Kayaga, Hashimu Juma Ismal, Jacok Qorro, Njomba Koi na Arcado Ntagazwa.

Waliogombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Wazee ni pamoja na Kwaio Hamis, Omary Masoud Omary, Suzan Lyimo (mbunge viti maalum), Clavery Ntidicha, Othma Haule na Omary Juma Mkama.

Pamoja na majina hayo, Benson alitaja majina na nafasi za wan
achama wao katika mabaraza wanayogombea nafasi ya katibu mhamasishaji, mweka hazina, wajumbe wa tano kuingia katika baraza kuu na wajumbe 20 kuingia mkutano mkuu wa taifa wa CHADEMA.

Hata hivyo, alisistiza kwamba, uchaguzi wa mabaraza utaanza Septemba 6 kwa Baraza la Wazee, Septemba 10 Bavicha na Bawacha Septemba 11 mwaka huu.

“Septemba 12 kamati kuu ya zamani itakaa kuandaa kikao cha Baraza Kuu jipya ambalo litakutana Septemba 13 kupitisha marekebisho ya vifungu vya katiba na kuandaa mkutano mkuu ambao utafanyika Septemba 14 mwaka huu.

“Baraza kuu litakaa tena Septemba 15 kwa ajili ya kutunga kanuni za kutekeleza vifungu vilivyopitishwa katika mkutano mkuu na kumchagua Katibu mkuu, Naibu katibu mkuu bara na visiwani pamoja na kuwachagua wajumbe wa kamati kuu,” alisema Benson.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

Habari na :-Tanzania Daima.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad