UTENDAJI KAZI CCM:-Makatibu wa mikoa 16 Wahamishwa Vituo,Bi.Janet Kayanda na Mushi wahamishwa Bukoba. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 04, 2014

UTENDAJI KAZI CCM:-Makatibu wa mikoa 16 Wahamishwa Vituo,Bi.Janet Kayanda na Mushi wahamishwa Bukoba.


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewahamisha  makatibu wake wa mikoa 16 kutoka katika vituo vyao vya kazi na mwingine  kupewa likizo ya miezi miwili. Uhamisho huo umesainiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Septemba 1 mwaka huu.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya chama hicho vimebainisha kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi na Uenenzi, Nape Nnauye, alipelekewa jalada namba CMMM/OKM/M.11/Vol.7/1/ ya ukurasa wa 106 na Katibu Mkuu wa chama hicho kujulishwa kuhusu uhamisho wa makatibu hao.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana

Janeth Kayanda.

Makatibu hao waliohamishwa  ni :-Joyce Masunga kutoka mkoa wa Mwanza kwenda  Pwani, Alphonce Kinamhala kutoka Katavi kwenda Arusha, Janeth Kayanda kutoka Bukoba Mjini kwenda Tabora na Gustav Muba kutoka Tanga kwenda Geita.

Wengine ni Katibu wa CCM  Pwani, Sauda Mpambalyoto ambaye anakwenda Kusini Unguja, Mary Chatanda kutoka Arusha kwenda Singida, Evelyne Mushi kutoka Kagera kwenda Katavi, Naomi Kapambala kutoka Singida kwenda  Kigoma.

 Idd Ame kutoka Tabora kwenda Kagera, Shija Othman Shija kutoka Kusini Pemba kwenda Tanga, Mwangi R. Kundya kutoka Mjini kwenda Mbeya, Mohamed Nyawenga anahamishiwa Mjini kutoka Kigoma, Adamu Ngalawa kutoka Shinyanga kwenda Mara.


Eveline Mushi (Kulia) akiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Constancia Buhiye.


Maganga Sengelema kutoka Mbeya kwenda Shinyanga, Mary Maziku kutoka  Geita kwenda   Dodoma na Bernard Nduta kutoka Dodoma kwenda Mwanza.
Aidha, Zainab Shomari aliyekuwa Katibu wa  CCM mkoa wa Kusini Unguja,  amepewa likizo ya miezi miwili.

Hata hivyo, uhamisho wa Mary Chatanda aliyekuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha umeelezwa kwamba huenda umetokana na yeye kudaiwa kujihusisha na vurugu zilizotokea jijini Arusha wakati wa uchaguzi wa Meya wa jiji hilo.

Uhamisho huo pia umezua maswali mengi kutoka kwa wanachama, mashabiki na wapenzi wa chama hicho wakihoji inakuwaje ufanyike katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu na mkuu mwaka 2015.

Kinana alipotafutwa kuelezea sababu za makatibu hao kuhamishwa simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) hakujibu.

Vilevile  Nnauye, alipotafutwa,  simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa na alipotumiwa sms hakujibu.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

Habari Na:-Nipashe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad