Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Septemba 3,2014 kuhusu
kupiga marufuku watu wanaotumia mitandao kinyume na taratibu.
Jeshi la Polisi nchini limetoa onyo
kwa watu wanaotumia mitandao vibaya ikiwemo kutuma ujumbe wa matusi, uchochezi,
picha za utupu sanjari na kukashifu viongozi wa Serikali, dini na watu
mashuhuri.
Akizungumza
Dar es Salaam, Septemba 3,2014 Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema
kuwa tayari baadhi ya watu wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu
tuhuma hizo na wengine wanaendelea kuhojiwa.
"Kumejitokeza
tabia kwa baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii na simu za kiganjani
kinyume na malengo yaliyokusudiwa kwa kusambaza taarifa za uchochezi,
kashfa,kuchafua viongozi wa Serikali."Wengine wamekuwa wanasambaza picha
utupu ambazo hazina maadili, hali ambayo ni kosa la jina, ingawaje mwingine
anaweza hasijue kuwa kufanya hivyo ni kosa lakini sheria haitamuacha, alisema.
Senso
aliendelea kubainisha kuwa kuvunja kutofahamu sheria kwa kutoifahamu si sehemu
ya kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria, atakabainika kutenda kosa hilo bila
kujali anaifahamu sheria au la, atachukuliwa adhabu kali.
Alisema oparesheni ya
kuwabaini wanaosambaza ujumbe zinaendelea nchi nzima kwa kushirikiana na
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kuwakamata waharifu wa aina
hiyo.
Aliongeza
kuwa hatua hiyo pia inawatia hatiani wale wote wanaotumia mitandao kufanya
utapeli na kujipatia kipato kwa watu mbalimbali nchini sanjari na blogs
zinazosambaza picha chafu ambazo ni kinyume na maadili."
Wapo baadhi
ya watu wanatumia mitandao ya simu kutapeli watu na kujipatia kipato, hivyo nao
ni sehemu ya waharifu wanaotafutwa na jeshi la polisi na yeyote atayekamatwa
hatua kali zitachukuliwa dhidi yake," alisema.
Hivyo
alisisitiza kuwa Jeshi hilo linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uharifu
huo, na kuwataka wale wanaotumiwa wa aina hiyo kutousambaza kwa wengine bali
waufute.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
|
No comments:
Post a Comment