RUSUMO CUP 2014 :-Watumishi FC waikacha Kago Stars katika Fainali ikichukua Ubingwa mbele ya Vijana kwa kuwafunga bao 1-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 12, 2014

RUSUMO CUP 2014 :-Watumishi FC waikacha Kago Stars katika Fainali ikichukua Ubingwa mbele ya Vijana kwa kuwafunga bao 1-0.

Katika fainali hiyo ya RUSMO CUP 2014 ambayo ilichezwa Jumapili Septemba 07,2014,katika uwanja wa shule ya msingi Nyakahanga mjini Rusumo na kushuhudiwa na mashabiki wengi ambapo Timu ya Wabeba Mizigo aka Kago Stars waliibuka Mabingwa wa Kwanza kwa kuwafunga Vijana Tegemezi bao 1-0.

Aidha  timu ya Watumishi FC waliofuzu kucheza fainali dhidi ya Kago Stars waliweka mpira kwapani kwa madai ya kukataa kuruhusiwa kuchezesha wachezaji iliyowasajili kutoka nje ya Kata ya Rusumo.

Akizungumza kabla ya kuhitimisha mashindano ya kuwania kombe la Rusumo kwa mwaka huu,Mjumbe wa NEC wilaya ya Ngara ,Issa Samma (anayetoa zawadi ya mpira) aliwataka Viongozi wa Vilabu na Vyama vya michezo wilayani Ngara mkoani Kagera  kudumisha Nidhamu ili kuleta chachu ya maendeleo ya michezo katika vilabu na vyama wanavyoviongoza.

Alisema ikiwa watakosa busara katika nafasi walizopewa na kuaminiwa kuziongoza ,kamwe wasitarajie kuwa na maendeleo katika sekta ya michezo.

Issa Samma ambaye alikua mgeni rasmi katika fainali hizo ambapo katika kutatua changamoto ya vifaa vya michezo,aliahidi kila timu shiriki kuipatia seti moja ya jezi.

Timu 6 zilishiriki Rusumo CUP 2014 ambazo ni Mshikamano FC,Kumubuga FC,Watumishi FC,Bodaboda FC,Wachenji Pesa FC na Mabingwa wa Ligi hiyo Kago Stars zote za kata hiyo na kufanikiwa kupata wachezaji 25 wanaunda timu ya kata hiyo.

Mjumbe wa NEC wilaya ya Ngara ,Issa Samma kulia akizindua T.Sheti za Klabu ya Rusumo FC anaefatia ni Kaimu Katibu mkuu wa Chama cha Soka wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bahati Kunzi.

Deusi Wistoni mchezaji wa Kago Stars akipewa zawadi yake ya ( Full Jezi ) ya ufungaji bora katika mashindano hayo na mgeni rasmi baada ya kufunga bao 6 kwenye Rusumo Cup 2014.
Mshindi wa kwanza ambaye ni Kago Stars ameondoka na zawadi ya Kikombe,Seti moja ya jezi na Mipira miwili huku Watumishi FC wakiambulia zawadi ya Seti moja ya jezi na mpira mmoja na kupitia kwa kiongozi wao wamejutia na kujilaumu kwa nini walishindwa kuzuia utovu wa nidhamu ulioibuka miongoni mwa wachezaji na kuwapelekea washindwe kucheza mchezo wa fainali dhidi ya Kago stars.


Muonekano wa Uwanja wa Shule ya Msingi Nyakahanga ambapo Kago Stars walionyeshana umwamba vilivyo dhidi ya Vijana Tegemezi na kufanikiwa kuwafunga bao 1-0 katika mchezo wa fainali ya  Rusumo Cup 2014.



Kutoka kushoto ni Mratibu wa Ligi ya Rusumo Cup 2014–Sulle Mohamed na Emanuel aka Manji wa Rusumo ambapo wamesema mashindano hayo ambayo yatakua endelevu,licha ya kufanikiwa kuimarisha undugu,umoja,kukuza mahusiano na kuibua vipaji vya wana Rusumo ,yalikumbwa na changamoto kwa timu shiriki kukosa vifaa vya michezo kama vile jezi na mipira na kuwaomba wadau wa michezo wilayani Ngara kusaidia timu kupata vifaa hivyo.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad