MAFANIKIO:-Watazame Wachezaji 31 wa kikosi cha Kocha Arsene Wenger wakiwa na mataji yao kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2005. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 12, 2014

MAFANIKIO:-Watazame Wachezaji 31 wa kikosi cha Kocha Arsene Wenger wakiwa na mataji yao kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2005.

Wachezaji 31 wa kikosi cha Arsene Wenger wakiwa na mataji yao kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2005.

 Klabu ya Arsenal imepiga picha ya kikosi chake kizima kipya wachezaji wakiwa na Kombe kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2005, The Gunners wakiwa wamepozi na mataji ya FA na Ngao ya Jamii.

Picha hiyo inahusisha wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu, sambamba na makinda waliopandishwa kutoka timu ya vijana. 

Danny Welbeck, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka Manchester United katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa pazia la usajili amesimama katikati ya wachezaji wenzake wapya Calum Chambers na beki kinda wa pembeni Hector Bellerin mstari wa pili, wakati Alexis Sanchez ni mchezaji pekee mpya aliyekaa mstari wa mbele.


Wachezaji wapya wa Arsenal, Mathieu Debuchy, Calum Chambers, David Ospina, Danny Welbeck na Alexis Sanchez.

Wachezaji wapya Sanchez na Welbeck wakiwa na kiungo mwenyeji kikosini Jack Wilshere (katikati) wakati wa upigaji picha. 

BPL-LIGI KUU ENGLAND-RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Septemba 13,2014.

1445 Arsenal v Man City

1700 Chelsea v Swansea

1700 Crystal Palace v Burnley

1700 Southampton v Newcastle

1700 Stoke v Leicester

1700 Sunderland v Tottenham

1700 West Brom v Everton

1930 Liverpool v Aston Villa

Jumapili Septemba 14,2014

1800 Man United v QPR

Jumatatu Septemba 15,2014

2200 Hull v West Ham

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad