Mhariri wa gazeti la Hoja, Yasini Sadick
(kushoto) akiwa na Neville Meena na Absalom Kibanda.
JUKWAA la
Wahariri Tanzania (TEF) limelaani tukio la Septemba 18,2014, la Polisi kuwapiga
waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHEDAMA), Freeman Mbowe, aliyefika Makao Makuu ya
Jeshi la Polisi kuhojiwa kuhusu madai ya kufanya maandamano nchini.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa TEF, Abasalom Kibanda, alisema miongoni
mwa waandishi waliopigwa, kujeruhiwa na kupoteza mali zao ni Yusuph Badi wa
magazeti ya TSN; Josephat Isango (Free Media) na Shamim Ausi (Gazeti la
Hoja) ambapo kuna wengi wengine ambao walipata usumbufu katika tukio hilo.
|
No comments:
Post a Comment