|
Pichani ni baadhi wadau kutoka Taasisi mbalimbali pamoja na watu wenye
ulemavu wa ngozi (Albinism) wakiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja huku
wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kuhamasisha amani nchini na
kupinga mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) nchini wakati wa
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika jana jijini Dar es
Salaam jana Septemba 21,2014.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
|
|
Meza kuu ikipoeka maandamano ya siku ya kimataifa ya amani kwenye viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Septemba 21,2014.
|
|
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi
akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi Mh. Seif Rashid (wa pili kulia).
Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,
Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Bw. Dunford Makala, Balozi wa Uturuki nchini, Mh.
Ali Davutoglu.
|
Wakati Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon anahimiza serikali
duniani kutafuta chanzo cha kukosekana kwa amani na kuongezeka kwa watu wenye
misimamo mikali, wasemaji katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa amani Duniani
wameitaka serikali ya Tanzania kutupia macho makali mauaji ya albino nchini.
Aidha Shirikisho
la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), limeitaka serikali
kupitisha adhabu ya kunyongwa kwa wale wanaohusika na mauaji ya Albino.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Amani Kimataifa ya Albino jana Septemba
21,2014,jijini Dar es Salaam, Rais wa Chama cha Albino Tanzania (TAS),Bw.
Joseph Tona, alisema kauli hiyo imetokana na ongezeko la idadi ya mauaji
dhidi yao.
Kadhalika, takwimu za kutoka mwaka 2006 zinaonyesha kuwa Albino 74
wameshauawa kikatili, huku 56 wakinusurika kifo, na kati yao 11 wameongezewa
ulemavu mwingine wa kudumu.
Alisema hofu
hiyo imesababisha maziko yao kutokuwa na heshima kama wengine kutokana na
baadhi ya familia kuwazika wapendwa wao kwa siri na wengine ndani ya nyumba, au
kuweka zege nzito katika makaburi kuzuia ufukuaji wa miili yao.
Alisema licha ya serikali kuweka vikosi kazi katika kudhibiti mauaji hayo, bado
haisaidii kitu kutokana na baadhi ya polisi na maofisa kuwa miongoni mwa vinara
wa kupokea rushwa.
Kwa mujibu wa Tona, matukio zaidi ya 120 ni kesi za mauji ya albino, kati yake
11 ndiyo yaliyofikishwa Mahakama, ambapo kati ya hizo kesi tano tu
zimeweza kutolewa hukumu hadi sasa.
|
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisoma
ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon kwenye maadhimisho ya
siku ya kimataifa ya amani duniani Septemba 21,2014, alisema ili kudumisha amani kuna
mambo mengi yanatakiwa kufanyiwa kazi hasa kutambua chanzo cha migogoro
inayosababisha msuguano mkubwa katika jamii na kukosekana kwa amani.
|
|
Mkurugenzi
wa Shirika la Under The Same Sun, Vicky Ntetema, aliishauri serikali
kupitia vikosi kazi vilivyochukua jukumu la kuchunguza mauaji na ukatwaji wa
viungo kwa albino, kutangaza matokeo kwa umma ili wahusika wachukuliwe hatua za
kisheria.
Pia, iuelezee umma matokeo ya kura za siri zilizopigwa katika mikoa tangu
mwaka 2009 hadi sasa zibainishwe wazi kwani nyingi zimeonyesha waganga wa jadi
kutumiwa na na viongozi wa kubwa katika kuwania nyadhfa mbalimbali serikalini.
Kutokana na hofu hiyo, ameitaka serikali kurejea mkakati wa mwaka 2009
uliotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ili kupiga marufuku
leseni za waganga wa kienyeji na wale wa jadi.
|
|
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid, akisoma hotuba kwenye maadhimisho ya
siku ya kimataifa ya amani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, alizitaka taasisi zilizopewa jukumu
la kusimamia vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya walemavu hususani albino
kutekeleza majukumu waliyopewa kisheria kwa uadilifu mkubwa jamii ya Watanzania
ione haki inatendeka ili kudumisha amani ya nchi.
|
|
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini
Tanzania (THBUB), Bi. Mary Massay akitoa nasaha kutoka kwa Tume hiyo, ambapo
alitoa rai kwa mtu yeyote yule ambaye ana malalamiko au matatizo katika Haki za
Binadamu anakaribishwa kwenye tume hiyo kwa ajili kupata msaada wa kisheria.
|
|
Akitoa
ushuhuda mmoja kati ya waathirika ambaye mikono yake miwili imekatwa, Mariam
Stanford, mkazi wa Ngara, mkoani Kagera, aliwataka wauaji wa albino wanyongwe
hadharani ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.
“Japokuwa Tanzania inasifika ndani na nje kama kisiwa cha amani, tafsiri hiyo
ni kinyume kwani ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa mauaji ya kikatili,
hivyo mwito wangu kwa viongozi wa dini tumieni midomo yenu kupinga hali hii kwa
sababu na sisi tumeumbwa na Mungu na tunastahili kuisha kama wengine,” alisema
Miriam.
Shuhuda aliyenusurika kwenye mauaji ya Albino ambaye amekatwa mikono yote
miwili, Mariam Stanford akitoa ushuhuda wake na killio chake mbele ya meza na
wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya
amani iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mnazi mmoja.
|
|
` Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE
SAME SUN, Vicky Ntetema akimfariji mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim
Davutoglu, wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani
iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar.
|
No comments:
Post a Comment