LIGI KUU TANZANIA BARA 2014/2015:-Wageni Ndanda FC Waanzia Kileleni Ligi kuu baada ya kushinda 4-1 dhidi ya Stand United. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 20, 2014

LIGI KUU TANZANIA BARA 2014/2015:-Wageni Ndanda FC Waanzia Kileleni Ligi kuu baada ya kushinda 4-1 dhidi ya Stand United.

Wageni wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2014/2015, Ndanda FC wameanzia kileleni kufuatia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji Stand United Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

MATOKEO MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA LEO SEPTEMBA 20,2014.

Azam FC 3-1 Polisi Moro

Stand United 1-4 Ndanda FC

Mgambo 1-0 Kagera Sugar

Ruvu Shooting 0-2 Prisons 

Mtibwa Sugar 2-0 Yanga SC

Mbeya City 0-0 JKT Ruvu

Maana yake, Ndanda FC wanaodhaminiwa na kampuni ya Bin Slum pamoja na Mbeya City na Stand United, wanakuwa wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa wastani wa mabao, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Azam FC walioshina 3-1 dhidi ya wageni wengine kwenye ligi hiyo, Polisi Morogoro. 

Mtibwa Sugar iliyoifunga mabao 2-0 Yanga SC Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ipo nafasi ya tatu sawa na Prisons ya Mbeya iliyowachapa wenyeji Ruvu Shooting mabao 2-0, wakati JKT Mgambo 1-0 iliyoilaza Kagera Sugar 1-0 ipo chini yao. 

Mbeya City iliyolazimishwa sare ya 0-0 na JKT Ruvu Uwanja wa Sokoine, Mbeya iko juu ya Yanga SC iliyolala 2-0 na timu nyingine zote zilizopoteza mechi leo Septemba 20,2014.

Ligi Kuu itaendelea kesho Septemba 21,2014,kwa mchezo mmoja kati ya Coastal Union ya Tanga dhidi ya wenyeji Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad