MWANASHERIA MAHIRI:-Hivi ndivyo Damas Ndumbaro alivyoibana Yanga SC na Emanuel Okwi kuwa Huru. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 08, 2014

MWANASHERIA MAHIRI:-Hivi ndivyo Damas Ndumbaro alivyoibana Yanga SC na Emanuel Okwi kuwa Huru.

Amechemsha?: Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji (kulia) siku alipotangaza kumshitaka Okwi. Kushoto ni makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga.

 Mwanasheria mahiri nchini, Dk Damas Daniel Ndumbaro, kwa mara nyingine ameonyesha umahiri mkubwa katika nyanja hiyo.

Dk Ndumbaro ambaye ni daktari wa sheria, mwalimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ndiye alikuwa akimtetea Okwi katika kesi dhidi ya Yanga iliyoamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, jana Septemba 07,2014.

Ndumbaro ambaye ni mwalimu wa katika Chuo Kikuu Huria (Out) aliwabana Yanga katika vipengele kadhaa na kuonyesha walivunja mkataba mapema.

Ameshinda? : Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe.

Taarifa zinaeleza kutokana na Dk Ndumbaro kuibana sana Yanga, ilifikia wakati mwanasheria aliyekuwa upande wa Yanga aliamua kutoa hoja kadhaa zikiwemo barua zao walizoziwasilisha TFF kuhusiana na kuvunja mkataba wa Okwi na ikawa sehemu ya kosa kubwa ambalo daktari huyo wa sheria alitumia kumaliza kesi.

Mwanasheria huyo ambaye ni kati ya wanasheria wachache nchini kuwa madaktari wa sheria, alimpa wakati mgumu mwanasheria wa Yanga na kuibana Yanga katika vipengele hivi


Mkali wa sheira?: Emmanuel Okwi (kulia) akiwaonesha ufundi wachezaji wa Gor Mahia siku ya jumamosi  Septemba 06,2014,uwanja wa Taifa, Simba ikishinda 3-0.

i) Yanga iliomba kuvunjwa mkataba wa Okwi bila ya kumpatia nakala, yeye akafanya juhudi ya kuzipata barua hizo na kukubaliana na hilo kwa barua pia, maana yake hakuwa tena na mkataba na Yanga.

ii) Yanga haikumalizia fedha zake dola 50,000 (Sh milioni 80), pia haikumlipa mshahara wa miezi mitano pamoja na nyumba, maana yake ilikiuka mkataba, hivyo ulishavunjika.

iii) Msisitizo bila ya kusema kiasi gani, Okwi naye anaidai Yanga fidia ya kukiuka mkataba ambao tayari umevunjika. Dk Ndumbaro ameitaka Yanga kumlipa mteja wake jumla ya shilingi milioni 111.8.

(Mchanganuo wa fedha hizo uko hivi; Fedha ya usajili dola 50,000 (Sh milioni 82.5), mshahara wa miezi mitano (kwa mwezi dola 3,000) dola 15,000 (Sh milioni 24.7) na kodi ya nyumba ya miezi 7, dola 400 kwa mwezi, jumla dola 2,800 (Sh milioni 4.6). Jumla ya zote ni Sh milioni 111.8.

Wametengana: Emmanuel Okwi (kulia) alicheza na Mganda mwenzake, Hamis Friday Kiiza wakiwa Yanga sc msimu uliopita 2013/2014.

Kutokana na ‘pini’ hizo za daktari huyo wa sheria maana yake, Okwi alikuwa huru, hivyo kamati hiyo inaweza kuendelea kujadili masuala mengine kuhusiana na ulipwaji wa fidia kutoka kwa kila upande kwenye kikao kingine.

HILI NDILO TAMKO LA YANGA SC .

Uongozi  wa klabu ya Yanga umesema utapinga maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji  kuhusiana na maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi kuwa huru.

Mwenyekiti wa Kamati  ya Sheria ya Yanga, Sam Mapande amesema kuwa hawajaridhishwa na maamuzi hayo ambayo yanakinzana na shitaka zima la mchezaji huyo.

Mapande amesema kuwa kamati ya TFF imeamua sakata la Okwi kinyume na malalamiko yao kwani hakukuwa na lalamiko la mchezaji huyo wa Uganda kuhusiana na malipo ya fedha zake za usajili.


Amesema kuwa cha kushangaza, kamati hiyo ya TFF iliamua kusikiliza kesi ambayo haikuwa mbele yao na kutoa maamuzi ambayo hata wao wameshangazwa nayo.

Amesema kuwa mazingira yalikuwa yameandaliwa kuibeba Simba na Okwi kwani hata malalamiko yao kwa Simba hayakusikilizwa.

Malalamiko yetu yalikuwa wazi kabisa, yapo kimaandishi, hatukuwai kulalamikiwa, suala la fedha za usajili la Okwi limetoka wapi, kama lilikuwepo, mbona hatujajulishwa kimaandishi kama utaratibu ulivyo,” amesema.

Amesema kuwa Kamati hiyo kumruhusu mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Zacharia Hans Pope ambaye pia ni mwenyekiti wakamati ya usajili ya Simba kuwemo katika kikao hicho kinyume na taratibu za Fifa kupitia kifungu namba 19 kinachoeleza mgongano wa kimaslahi.


Na:-SaleheJembe.com
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad