MUENDELEZO WA AJALI YA BASI LA AIR BUS:-Tazama Picha 4 Lilivyoharibika Vibaya chanzo kikiwa ni Mwendo Kasi na kuua Watu 4 Papo Hapo leo Septemba 08,2014 mkoani Morogoro. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 08, 2014

MUENDELEZO WA AJALI YA BASI LA AIR BUS:-Tazama Picha 4 Lilivyoharibika Vibaya chanzo kikiwa ni Mwendo Kasi na kuua Watu 4 Papo Hapo leo Septemba 08,2014 mkoani Morogoro.


Watu wanne wamefariki dunia  baada ya basi la kampuni ya Air Bus kuacha njia na kutumbukia katika daraja la Mkange eneo la Berega nje kidogo ya mji wa Morogoro katika barabara kuu ya Morogoro- Dodoma leo September 08,2014 asubuhi.


Picha zote Na:-Mwanawamakonda WhatsApp +255789925630.


Akiongea na Waandishi wa Habari, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro,Leonard Paulo  aliyefika eneo la tukio amesema kuwa Ajali hiyo imejeruhi Wanaume 18 na Wanawake 10 waliolazwa Hospitali ya Barege kwa Matibabu.

Amesema kuwa chanzo cha Ajali hiyo ni  mwendo kasi wa dereva wa basi hilo ambaye alikimbia baada ya ajali, huku mashuhuda nao wakieleza namna walivyowaokoa majeruhi ambao walirushwa chini kupitia kwenye vioo na wengine walinasa kwenye siti za abiria.

Basi hilo aina ya Scania namba T 106  AGB  lilikuwa linatoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Tabora, limeharibika vibaya baada ya kuangukia chini ya daraja la mto Mkange ambao hauna maji.

Aidha mganga mfawidhi wa hospitali ya Berega Dk Alfred Chiponda akithibitisha kupokea majeruhi 34 ambao baadhi yao wamevunjika miguu na mikono na miongoni mwao watapelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu.

Kumekuwa na mfululizo wa ajali za barabara zinazogarimu maisha ya watu ambapo hivi karibuni kumetokea ajali mkoani Mara ambapo watu 36 walifarikii dunia papo hapo na wengine wawili wakafariki hospitalini huku ikiacha wengine wengi na vilema vya kudumu.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad